Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye yuko katika ziara ya kitaifa nchini Tanzania akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es Salaam ambapo alipokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Juni 20, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye yuko katika ziara ya kitaifa nchini Tanzania  wakipokea heshima ya wimbo wa taifa mara baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es Salaam Juni 20, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongozana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye yuko katika ziara ya kitaifa nchini Tanzania baada ya kumpokea alipowasili ikulu jijini Dar es Salaam Juni 20, 2026