Mkurungezi msaidizi wa afya ya mtoto na vijana kutoka wiraza ya Afya, Dkt Felix Bundala mwenye kati njeusi aliyekaa katikati akiwa kkwenye picha ya pamoja na wataalum wa afya kutoka mikoa mitano ya Tanzania bara.
Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto kutoka mkoa wa Tabora Audrey Bakuza akiwasilisha maoni ya mkoan wa tabora katika kikao cha utekelezaji wa kitita cha uzazi salama
Mkurungezi msaidizi wa afya ya mtoto na vijana kutoka wiraza ya Afya, Dkt Felix Bundala aliyekaa katikati mwenye koti njeusi katika picha ya pamoja na waratibu wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto kutoka mikoa ya Manyara, Shinyanga, Mwanza, Geita, na Tabora.
……………………….
Na Lucas Raphael Tabora
Mkurungezi msaidizi wa afya ya mtoto na vijana kutoka wiraza ya Afya, Dkt Felix Bundala imewataka watoa huduma katika mikoa mitano ya Tanzania ambayo imebainishwa kuwa na vifo vingi vya watoto wakati wa kuzaliwa kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake kwa lengo la kupunguza vifo ambayo ndio kampeni ya uzazi salama ni kipaumbele cha Dunia nzima .
Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kikao cha utekelezaji wa kitita cha uzazi salama kwa waganga wa mikoa mitano ya Tanzania bara kilichofanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora .
Dkt Felix Alisema kwamba watoa huduma katika mikoa mitano iliyobainishwa kuwa na vifo vingi vya watoto wakati wa kuzaliwa wanapaswa kutoa huduma bora ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi .
Alisema kwamba kitita cha uzazi salama lengo lake ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga ndani ya saa 24 hadi siku saba .
Alisema kwamba waganga wa mkoa ,wilaya , waratibu wa afya ya uzazi na mtoto na watoa huduma wanatakiwa kutoa huduma iliyobora ili kuokoa maisha ya watoto wachanga wanapozaliwa .
Alisema kwamba Kitita cha uzazi salama ni jumuisho la mbinu kadhaa za kuboresha afya kwa kupunguza vifo vya mama na watoto wakati na baada ya kujifungua.
Awali akizungumza katika kikao hicho cha utekelezaji wa kitita cha uzazi salama ,mtafiti mwandamizi kutoka hospital ya Haydom Dkt Benjamini Kamala alisema kwamba mradi huu uliundwa baada ya matokeo ya tafiti zilizofanyika katika hospitali ya kilutheri ya haydom kitengo cha utafiti kwa zaidi ya miaka 10 na kuthibitika kuwa mchango wake katika kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Alisema kwamba mradi ulijikita zaidi katika kumwongezea ujuzi mtoa huduma kwa kumwezesha kugundua kwa haraka dalili hatarishi za mama kipindi akiwa katika uchungu ili aweze kujifungua salama.
Aliongeza kusema kwamba kumwongezea mtoa huduma ujuzi wa kumsaidia mtoto mchanga anayeshindwa kuanza kupumua mara baada ya kuzaliwa.
‘’kuboresha huduma, uwezo wa kutathimini maendeleo ya uchungu, hali ya mtoto mchanga kabla na baada ya kuzaliwa, kumsaidia mtoto mchanga kupumua pale inapohitajika na kumsaidia mama asipoteze damu nyingi baada ya kujifungua vitaimarika zaidi. “alisema Dkt Kamala.
Mratibu wa mradi kitita cha uzazi salama Ivony Kamala alisema kwamba mradi unatekelezwa katika hospitali na vituo vya afya 30 katika mikoa mitano ambayo ni Manyara, Shinyanga, Mwanza, Geita, na Tabora.