Makamu Mwenyekiti-ULINGO, Bi.Nancy Mrikaria akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitoa pongeza kwa Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini. Makamu Mwenyekiti-ULINGO, Bi.Nancy Mrikaria akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitoa pongeza kwa Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini. Makamu Mwenyekiti-ULINGO, Bi.Nancy Mrikaria akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitoa pongeza kwa Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini.Mwenyekiti wa UWT Kinondoni Bi.Anna Hangaya akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitoa pongeza kwa Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini. Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Bi.Saum Rashid akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitoa pongeza kwa Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini. Baadhi ya wanajumuiya wa ULINGO wakiwa katika Mkutano na waandishi wa habari kumpongeza Rais Samia kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya hadhara nchini.
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BAADA ya Rais Samia Suluhu kutoa rukhsa kufanyika kwa mikutano ya hadhara hivi karibuni, Jumuiya ya Wanawake Wanasiasa Nchini (ULINGO) wamepokea kwa mtazamo chanya suala hilo kwani linawaimarisha Watanzania ambao ni wanawake na wanaume kuweza kushiriki kwenye siasa bila vurugu.
Ameyasema hayo leo Januari 6,2022 Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti-ULINGO, Bi.Nancy Mrikaria wakati walipokutana jumuiya hiyo na waandishi wa habari kutoa mtazamo wao kuhusu masuala ya kisiasa.
Amesema wamewapongeza viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kwa kutoa maoni yao kwa wakati tofauti hatua iliyopelekea Mh. Rais na serikali yake ya awamu ya sita kuwa sikivu na kufanyia kazi suala la mikutano ya hadhara ambalo ilitolewa maoni na kikosi kazi cha Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoongozwa na Profesa Rwekaza Mukandala na kamati maalumu ya Zanzibar ya Mhe. Rais Dkt Hussein Ally Mwinyi iliongozwa Dkt Ally Uki, ambapo kwa pamoja walipendekeza mambo
mbalimbali ikiwemo suala la mikutano ya hadhara.
“Tunatumia fursa hii adhimu tuliyoipata leo kumpongeza kwa kazi kubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo, ambayo ameifanya kwa ubunifu mkubwa sana, Taifa linazidi kuimarika kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia”. Amesema
Aidha wamemuahidi Rais Samia kumpa ushirikiano wa kutosha bila kujali itikadi za vyama vyao kwenye suala zima la kuendeleza, kudumisha na kulinda msingi wa Tunu ya Taifa wa AMANI na UTULIVU uliopo nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Kinondoni Bi.Anna Hangaya amesema jambo ambalo amelifanya Rais Samia ni jambo ambalo limemgusa kila mwananchi kwani tunapenda umoja hivyo basi viongozi wa juu wakishikamana tunaamini huku chini watakwenda vizuri.
Amesema Rais Samia kuachilia mbali suala la kuruhusu mikutano ya hadhara, amefanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta ya Afya mbayo imekuwa ni muhimu kwa kila mwananchi.
Nae Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Bi.Saum Rashid amewataka wanasiasa kufanya mikutano kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, wasilete taharuki kwa wananchi bali waendeshe mikutano kwa amani na utulivu ili kuendeleza mshikamano kwa wananchi kwa ujumla.