Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi Dkt. Angelina Mabula amesema mwaka 2022 Shirika la Taifa la Nyumba NHC limeweza kutelekeza miradi mbali mbali na kuhuwisha sera mbali mbali ikiwa na ni pamoja na miradi ya ukadarasi ikiwemo ujenzi wa majengo ya ofisi za Wizara Nane(8) katika mji wa serikali Dodoma yenye Jumla ya Bilion 186.8.3.
Amesema miradi iliyotelekezwa ni pamoja ujenzi ofisi ya Wizara ya madini, ofisi ya Wizara ya mifugo na uvuvi, ujenzi wa ofisi Wizara ya Utamaduni na michezo, Wizara ya mambo ya Ndani, Wizara ya habari na technolojia ya habari, Wizara ya Nishati na Wizara ya Ardhi nyumba na makazi huku miradi hiyo ikitarajiwa kuisha June 2023.
Waziri Dkt. Mabula amyeasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ardhi mkoa zilizoko Posta jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na waandishi wa habari katika kuelezea mikakati ya wizara hiyo katika maendeleo.
Aidha shirika linaendelea na ujenzi wa jengo la shule ya uchumi katika chuo kikuu cha Dar es salam, ujenzi wa majengo matano ya wakala wa ununuzi wa Serikali, ujenzi wa jengo la Tanzanite mirerani, ujenzi wa kitengo cha moyo Jakaya kikwete.
Ameongeza kuwa shirika hilo pia linaendelea na utelekezaji wa mradi wa nyumba za makazi elfu tano(5000) za gharama za kati za miradi ya chini ya mradi wa “Samia Housing Scheme” ambapo asilimia 50% ya nyumba hizo zitajegwa Dar es salam, Dodoma asilimia 20%, na mikoa mingine itajegwa asilimia 30%, nyumba hizo zimeanza kujengwa mwezi Septemba eneo la Kawe jijini Dar es Salaam na mradi huo utatekelezwa kwa awamu ukigharimu shilingi Bilion 466 sawa na Dolla za kimarekani milion 200.
Hata hivyo shirika hilo limekamilisha ujenzi wa nyumba mia tatu (300) Iyumbu Dodoma pamoja mia moja(100) eneo la Chamwino huku wakieleza kwamba nyumba hizo ni kwa ajili ya kuuzwa.
Kuhusu utayarishaji wa sera ya ubia shirika limeweza kuhuisha, kuitayarisha na kuzindua sera ya ubia ili kushirikisha wadau mbalimbali kuendeleza sekta ya makazi na kuongeza makazi bora kwa ajili ya Watanzania ambapo sera hiyo ilizinduliwa tarehe 16 Novemba 2022 na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Aidha katika suala la ukusanyaji kodi shirika limefanya kampeni katika kukusanya malimbikizo ya wadaiwa Sugu hadi sasa shirika limeweza kukusanya shilingi Bilion 5 na linaendelea na hatua mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba na wapangaji na kuruhusu madeni kulipwa kwa awamu, shirika pia linakusudia kuvunja mikataba ya wapangaji waliokaidi kulipa madeni yao kwa kuwaondoa kwenye nyumba na kuchukua mali zao na kuziuza ili kufidia madeni wanayodaiwa.