Bado changamoto ya mimba mashuleni pamoja na utoro uliokithiri wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe umeendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya taaluma jambo ambalo linamsukuma mkuu wa wilaya hiyo Comrade Ally Kassinge kutoa mikakati 20 ya kukabiliana na hali hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu za idara ya elimu illiyotolewa na afisa elimu sekondari Loice Mgonja na msingi Fredrick Mhanze wilayani humo imebainisha wanafunzi 22 walikatishwa masomo mwaka jana huku kuanzia januari 2019 hadi sasa wanafunzi 6 wamekatishwa masmo huku pia kuhusu utoro ikielezwa wanafunzi 166 hawakuripoti shule 2018 na wanafunzi 187 kwa 2019 jamno ambalo linaisukuma serikali kuchukua hatua .
Kufuatia ripoti hiyo ya mikasa ya mimba na utoro mkuu wa wilaya ya hiyo comrade Ally Kassinge anachukizwa na kutoa mikakati 20 ya kudhibiti mimba wilayani kwake na kuahidi kuanza kuwafatilia wanaume waliosababisha mimba mashuleni pamoja nawazazi walikwamisha watoto wao kuendelea kidato cha kwanza.
Nao baadhi ya wadau wa elimu ambao wameshiriki katika kikao cha cha tathmini ya elimu akiwemo Ibrahim Chengula wanakiri wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto kubwa ya wazazi kushinikiza watoto wao kujiferisha mitihani na kuhitaji hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe ni miongoni mwa halmashauri mbili za mwisho kitaaluma kati ya 6 za mkoa wa Njombe 2019.