Home Mchanganyiko BEI YA MIFUKO MBADALA YA PLASTIKI KIKWAZO KWA WANUNUZI NA WAFANYABISHARA NJOMBE

BEI YA MIFUKO MBADALA YA PLASTIKI KIKWAZO KWA WANUNUZI NA WAFANYABISHARA NJOMBE

0

NJOMBE

Ikiwa siku nne zimesalia kuanza kutekelezwa kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki nchini,wafanyabiashara wakubwa wa mifuko hiyo mjini Njombe wameiomba serikali kuwaongezea muda wa kutekeleza katazo hilo ili kuwaepusha na hasara kwani bado wanahazina kubwa gharani.

Wakizungumzia mwamko wa wateja katika kununua vifungashio vipya baadhi ya wafanyabiashara wa mifuko ya plastiki akiwemo Asia Mgaya, Oneva Ilomo na Matrida Sanga wanasema mwamko umekuwa mdogo kwasababu vifungashio hivyo vimekuwa vikiuzwa kwa bei ya kuanzia elfu 2 hadi elfu tatu hatua ambayo inawafanya wateja kuacha kununua bidhaa kutokana na kukosa fedha ya kununua kifungashio.

Matumizi ya mifuko ya plastiki nchini yamekuwa yakifanyika vizazi na vizazi lakini katazo la serikali limepokelewa vipi na wananchi ambapo Ester Kiswaga,Upendo Julias wanasema wamekuwa wakilazimika kubeba mikononi bedhaa zao kwasababu ya kukosa fedha za kununua mifuko hiyo ambayo inauzwa kuanzia shilingi mia 2 hadi mia 5

Nae Betrice Sanga ambaye ametumia katazo hilo kuwa fursa amebuni mradi wake vikapu mjini Njombe na kupata mwamko mkubwa wa wateja hapa anatoa mtazamo wake kuhusu ujasiriamali wake ambapo anaomba serikali kumuwezesha mtaji ili kufanya uzalishaji mkubwa .