………………………
Wadau wa sekta binafsi, mazingira, vituo vya utafiti pamoja na vyuo vikuu nchini wametakiwa kuweka nguvu zaidi kuhakikisha wanaendeleza ajira endelevu za kimazingira ili jamii iweze kuzitambua na kusaidia kuondoa ombwe iliopo ya ukosefu wa ajira kwa vijana.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaa Desemba 21, 2022 katika uzinduzi wa matokeo ya Utafiti uliolenga kuangalia changamoto zilizopo katika fursa kwa vijana hususani zinazolenga uendelevu wa matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira.
Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa Miradi kutoka shirika la Mtandao wa Mabadiliko tabia nchi Forum CC Msololo Onditi amesema kumekuwa na uelewa mdogo juu ya ajira endelevu za kimazingira, sera na ushiriki wa sekta binafsi ukitajwa kuzorotesha fursa hizo kufikiwa.
Kwa upande wake Afisa mratibu tafiti mwandamizi COSTECH Dkt. Prosper Masawe amesema Mashirika na asasi za kiraia zimetajwa kuwa na mchango kubwa katika kuchagiza uelewa kwa vijana fursa zilizopo kwenye ajira zisizoathiri mazingira ili kuondoa changamoto ya ajira na mabadiliko ya tabia nchi huku wakiendelea kutunza mazingira.
Utafiti huo ulitekelezwa katika wilaya za Kilwa, Kibondo, Kasulu Mkoani Kigoma na Wilaya ya Singida na Tanga ambapo pia Vijana wametakiwa kutunza mazingira wanayoishi kwani yana fursa za kutoa ajira ikiwa watazingatia shughuli endelevu katika mazingira.
Mwisho.