Julius Ruwaichi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access kikabidhi msaada wa vifaa vya kujifungulia kwa akina Mama kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali Rufaa mkoa wa Temeke Dkt Joseph Gasper Kimaro ikiwa na kurudisha shukurani kwa jamii kushoto ni Nuswe Ambokile Muuguzi Mkuu Hospitali ya Rufaa mkoa wa Temeke.
………………………
Akizungumza na waandishi wa habari Julius Ruwaichi mkurugenzi mtendaji wa Bank ya Acess amesema kuwa wametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia kwa akina Mama katika hospital ya Temeke ikiwa na kurudisha shukurani kwa jamii.
Leo tumetoa mchango wetu ikiwa ni kurudisha shukurani kwa jamii na kuendelea kujali Afya kwa mama na mtoto na huu ni sehemu ya mpango wetu wa kimkakati kuendelea kuwa na jamii katika kuboresha Afya ya jamii.
Amesema Julius.
Julius ameongeza kwamba Access Microfinance Bank ilianza Biashara hapa nchini mwaka 2007 na tawi Lao la kwanza lilikuwa katika wilaya ya Temeke.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke Dkt Joseph Gasper Kimaro amesema kwamba anawashukuru benki ya Access kwa kuitembelea hospitali hiyo na kuleta msaada huo na kuahidi kuwafikishia wakina mama wajawazito ambapo wana uhitaji mkubwa wa vifaa hivi na utakuwa ni msaada mkubwa sana kwao.
Aidha Dkt Kimario ameongeza kwamba wakina Mama mia saba(700) wanajifungua katika hospital hiyo huku wakina mama mia mbili hamsini(250) hadi mia tatu (300) wanajifungua kwa njia ya kawaida.
Pamoja na kupokea kutoka kwenu Access Bank napenda kuchukua fursa hii pia kuwashawishi wadau waweze kufuata mfano wenu kurudisha kwa jamii kwani inakuwa ni sadaka iliyo bora. Amesema Dkt Kimario.
Dkt Kimario ametumia nafasi hiyo pia kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita kupitia Wizara ya Afya kufanya uwekezaji mkubwa ikiwa ni kukarabati baadhi ya Majengo na kuongeza vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali Rufaa mkoa wa Temeke Dkt Joseph Gasper Kimaro akipokea vifaa vya kujifungulia akina mama katika hiyo kutoka kwa Bi. Tunu Lwoga Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi Benki ya Access ikiwa na kurudisha shukurani kwa jamii kushoto ni Nuswe Ambokile Muuguzi Mkuu Hospitali ya Rufaa mkoa wa Temeke.
Mganga Mfawidhi wa hospitali Rufaa mkoa wa Temeke Dkt Joseph Gasper Kimaro akipongezana na Julius Ruwaichi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access mara baada ya makabidhiano hayo.
Julius Ruwaichi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access akikabidhi vifaa hivyo kwa Christina Cleofas mmoja wa akina mama wajawazito katika wodi hiyo.
Nyemo Kongole Muuguzi Mkuu wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali hiyo akiishukuru uongozi wa benki ya Access kwa msaada huo