Bw. Habibu Mchange Mwenyekiti wa Kituo Cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na taarifa MECIRA akiwasilisha taarifa yake kwenye Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji linalofabyika kwenye ukumbi wa Masiti Gangilonga Mkoani Iringa Leo Disemba 19,2022 ambapo Mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdori Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifuatilia taarifa ya Bw. Habibu Mchange Mwenyekiti wa Kituo Cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na taarifa MECIRA kwenye Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji linalofabyika kwenye ukumbi wa Masiti Gangilonga Mkoani Iringa Leo Disemba 19,2022 kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Halima Dendego.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiteta jambo na Bw. Habibu Mchange Mwenyekiti wa Kituo Cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na taarifa MECIRA kwenye Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji linalofabyika kwenye ukumbi wa Masiti Gangilonga Mkoani Iringa Leo Disemba 19,2022.
Wadau mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo.
……………………………..
Na Fredy Mgunda, Iringa
ZAIDI ya siku 130 mto Ruaha mkuu (Great Ruaha) haujatiririsha maji kutokana na uharibifu wa bonde la Ihefu unaofanywa na baadhi ya wananchi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Akizungumza wakati wa kongamano la wahariri na wadau wa uhifadhi, mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji, Mwa MECIRA Habibu Mchange amesema kuwa shughuli za kibinadamu zinazofanywa na wananchi wachache katika bonde la Ihefu ndio wamekuwa chanzo cha kukauka kwa Mto Ruaha.
Mchange amesema kuwa kutokana na uharibifu huo kumepekea wanyama wengi katika hifadhi ya Taifa Ruaha kufa na wengine kuambukizwa magonjwa mbalimbali kutokana na kukosa maji ya kutosha.
Ameongeza kuwa serikali inatakiwa kuchukua hatua kali kwa wananchi wote ambao wamekuwa wakiharibu mazingira ili kunusuru wanyama waliopo katika hifadhi ya Taifa Ruaha
Mchange amtanabaisha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya ardhi ya Tanzania imeharibika na asilimia 16 ya nchi ya Tanzania ni Jangwa kutoka na uharibifu wa kimazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi.
“Mto Ruaha na mito mingine kama hatua za haraka hazitachukulia basi tutavuna mabua kutokana na uharibifu unaoendelea,” Amesema Mchange
Mchange aongeza kuwa zaidi ya hekari laki nne za misitu zimeharibiwa na baadhi ya wananchi wasiokuwa na mapenzi ya nchi yao hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo.
Amemalizia kwa kusema kuwa waandishi wa habari wapo tayari kuisaidia serikali kuibua na kuandika habari za kuelimisha na kuwafichua waharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.