Kamishna wa uhifadhi wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services agency (TFS) Prof DoS Santos silayo akizungumza kando ya kongamano mazingira linalofanyika mkoani Iringa eo.
………………………
Na Fredy Mgunda, Iringa.
KAMISHINA wa uhifadhi wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services agency (TFS) Prof. DoS Santos Silayo amewata wakulima kulima na kutunza mazingira ili kuendelea kupata mvua za kutosha.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati kongamano la wahariri na wadau wa uhifadhi, mazingira nabutunzaji wa vyanzo vya maji, Prof Silayo alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuendelea kuvitunza vyanzo vya maji na mazingira kwa faida ya Taifa na dunia kwa ujumla.
Prof. Silayo alisema kuwa wakulima na wafugaji wamekuwa wakiharibu mazingira na vyanzo vya maji kwa kilimo na ufugaji ambao hauna tija kwa wananchi wengi kwa kuwa wamekuwa wakiharibu mazingira bila sababu ya msingi.
Aliwataka wananchi kupinga vikali kwa wananchi wengine ambayo wamekuwa wakiharibu mazingira kwa makusudi na kusababisha majanga kwa binadamu na wanyama.
Prof Silayo alisema kuwa mazingira yakitunzwa vizuri yanakuwa na faida kubwa katika maisha ya binadamu na viumbe vingine ambavyo kwa kiasi kikubwa wanategemea mazingira mazuri na bora.
Alimazia kwa kusema kuwa ukitunza mazingira vizuri na mazingira yatakutunza hivyo jukumu la kutunza mazingira ni jukumu la kila wananchi.