MKUU wa MKOA wa Tabora Dkt Balozi Batilda Buriani akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani mkutano ulifanyika leo mbele ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa Tabora .
………………….
Na Lucas Raphael Tabora.
Mkoa wa Tabora kesho unatarajia kuzindua kampeni iliyopewa jina la ‘Kijana zungumza na mkuu wa mkoa” yenye lengo la kuwasikiliza vijana na kuwapa mbinu za kuwapa fursa za kujiinua kiuchumi
Akizungumza leo ,mkuu wa mkoa wa Tabora,Dk Batilda Burian,alisema wanatarajia kuwa na kundi kubwa la vijana kesho ambalo litasikilizwa na kupewa mbinu za kufahamu fursa mbalimbali ili wazitumie na kujiinua kiuchumi.
Dk Burian alisema wanataka vijana waondokane na tabia ya kulalamika kutokuwa na shughuli za kufanya kwani zipo nyingi na kinachotakiwa ni kuwaonesha fursa hizo na namna ya kuzitumia.
Alieleza kuwa watakuwa na wataalamu mbalimbali na watazungumzia Vijana na uwekezani,Siasa na uchumi kilimo,uvuvi,ufugaji na shughuli zingine nyingi lengo pia likiwa ni kujenga kizazi bora cha kesho.
Alisema wanataka ndani ya miezi mitatu kuanze kuonekana mabadiliko na kwamba kampeni hiyo anataka.ilete mabadiliko ya maisha ya vijana na wakazi wa mkoa wa Tabora kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Viva Promotion Company ltd,inayojishughulisha na uchapishaji,Sylvester Geneli,alisema hiyo ni fursa adhimu kwa vijana katika kufahanu fursa na namna ya kuzitumia kujiinua kiuchumi.
Naye mkurugenzi wa Madam Vai Investment,Violate Lusana,alieleza kuwa kampeni hiyo ni muhimu na itakiwa na manufaa makubwa kwa vijana.