…………………..
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi nchini, Bw Adrian Nyangamale ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Mawasiliano Serikalini ya Wizara hiyo Kwa kuibuka Mshindi wa nne kwa Utoaji wa Habari sahihi za Wizara kwa umma katika sekta ya Maliasili na Utalii ambayo imekua na mchango mkubwa katika maendeleo ya Sanaa za ufundi nchini.
Aidha Bw Adrian ameongeza kuwa, tuzo hiyo ni matokeo chanya ya utendaji kazi mzuri wa Maafisa Habari wa Wizara hiyo unaosaidia kuifanya jamii kuwa na uwelewa mpana wa utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Wizara hiyo hasa zinazofanywa na Viongozi wake wa Juu.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa na anaendelea kufanya kazi kubwa sana katika sekta ya Maliasili na Utalii, kazi inayoendelezwa vizuri na Viongizi na watendaji wa Wizara, hapa Idara ya Habari imeiheshimisha Wizara na imeiheshimisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi, nashauri kazi iendele Kwa Kasi zaidi” Aliongeza Bw. Nyangamale.
Ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo ndiyo yenye dhamana ya Maliasili na Utalii ni kikonyo na mdau mkubwa wa Sanaa za Ufundi nchini akitoa mfano wa Sanaa ya Uchongaji ambazo kwa asilimia kubwa zinategemea Wizara hiyo kupitia malighafi za mazao ya misitu ambayo yanasimamiwa na sekta ya Maliasili na soko lake kubwa ni watalii.
“Mafanikio ya Wizara hii ni mafanikio makubwa ya tasnia ya Sanaa za Ufundi nchini kwani kwa kutoa habari za uhakika kwa umma inasaidia jamii kuwa na uelewa mpana juu ya kazi na jukumu la Wizara ikiwemo kutekeleza Mipango Mikakati ya kutunza na kulinda Maliasili zetu sanjari na kutangaza vivutio vyetu jambo linasaidia pia wadau na wanufaika wengine wakiwemo Wasanii wa Sanaa za Ufundi, kuwahakishia uwepo wa malighafi na upatikanaji wa soko la Sanaa hii ndani na nje ya nchi” Amesisitiza Adrian.
Wizara ya Maliasili na Utalii leo Desemba 17, 2022 imepata Tuzo ya mshindi wa nafasi ya nne kwa utoaji wa habari sahihi za Wizara kwa umma katika sekta ya Malisili na Utalii na utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa mwaka 2022, imetolewa katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari nchini mwaka 2022 Jijini Dar es Salaam.