Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza alipokuwaakitoa mada katika Mkutano wa viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania na Wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika leo Disemba 16,2022 katika kituo Jumuishi cha utoaji Haki Jijini Far es Salaam.
Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Sylvester Kainda akitoa mada kuhusu uendeshaji wa mashauri katika mahakama katika Mkutano huo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), akiwa na Mkuu wa kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania Dkt. Angelo Rusha (kulia) wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Sylvester Kainda
Badhi ya Wahariri wa habari wakifuatilia Mkutano huo
Mkuu wa kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania Dkt. Angelo Rumisha akiwasilisha mada kwenye Mkutano huo.
Akizungumza na Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanania TEF Mtendaji Mkuu wa mahakama Tanzania Profesa Elisante ole Gabriel wakati akifungua kikao kazi cha viongozi waandamizi wa mahakama ya Tanzania na wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika kwenye kituo cha IJC Temeke Jijini Dar es salam leo, amesema kwamba wahariri wanatakiwa kujifunza na kujua namna gani Mahakama nchini zinavyofanya kazi na kuelewa uongozi wa mahakama unavyotenda kazi na wahusika katika vitengo mbali mbali kumsaidia mwandishi au mhariri endapo ana shida ya kikazi aweze kujua ni nani mhusika wa jambo hilo kitu ambacho kitakuwa rahisi katika kazi na kuwezesha kutoa taarifa zenye uhakika.
Ameongeza kwamba wahariri na waandishi kujua uongozi wa mahakama na vitengo vyake vya kazi itasaidia kuondoa misuguano kati ya mahakama na vyombo vya habari.
Tanzania ina Hatua tano(5) za mahakama ambayo ni Mahakama ya Rufaa, Mahakama kuu, Mahakama za hakimu mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo.
Wahariri na waandishi wanatakiwa kujifunza ili kupitia vyombo vyao waweze kutoa elimu kwa wanachi kuelewa namna ambavyo kila Ngazi ya mahakama inafanya kazi zake kuepusha malalamiko ambapo kwa mujibu wa sheria za mahakama kesi inayowasilishwa kwenye mahakama ya mwanzo inatakiwa isizidi miezi sita(6) bila kusikilizwa, huku mahakama ya Rufaa kesi haitakiwi izidi miezi ishirini na nne(24).
Ni vyema mkasoma na mkaelewa namna mahakama zetu zinavyofanya kazi ili muweze kwenda kuandika habari zenye uhakika kuepusha ukakasi kwenye jamii. Amesema Profesa Elisante.
“Lakini sambamba na hilo haya mabadiliko na maboresho yasingefanyika bila rasilimali fedha , tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake hususani Wizara ya Fedha chini ya Waziri Dk.Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu Emaenul Tutuba kwa jinsi ambavyo tukihitaji rasilimali fedha wanatupatia kwa wakati ili kufanikisha haya maboresho na jengo la makao makuu ya mahakama linalojegwa Dodoma limegharimu Bilioni 129.7.
Amesisitiza wanapohitaji rasilimali fedha wamekuwa wakipatiwa kwa wakati na kwamba wanatamani wananchi wazidi kupata huduama kwa haraka huku akieleza Mahakama ya sasa ni ya Kidigiti.
Kuhusu kuhamia Dodoma , Profesa Gabriel amesema Serikali imeendelea kuwawezesha, hivyo jengo la Mahakama linaendelea vizuri na mpango wao uko pale pale watalipokea jengo mwishoni mwa Desemba ili taratibu nyingine za kuweka samani ziendelee.
“Jengo lile litakuwa la sita kwa ukubwa duniani kwasababu litakuwa na ukubwa wa Squre mita 60,000 na niseme lina matawi matatu makubwa, moja ni la Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na Mahakama ya Juu , na kutakuwa na jengo la utawala pale katikati.Watu wengi wanajiuliza kwenye Katiba kwamba Mahakama ya Juu haipo, ndio kusema tunawashukuru sana viongozi wetu wakati maboresho haya yanafanyika Balozi Hussein Katanga pamoja na Jaji Othman Chande.
“Walisema katika mchoro iwepo Mahakama ya Juu hata kama kwa sasa haijaanza kutumika ili itakapoanza tusiingie gharama za ujenzi, niseme tu wakati huo utakapofika kwa kuwa miundombinu ya majengo yatakuwepo kwa ajili ya Mahakama ya Juu hivyo Serikali itawezesha masuala ya rasilimali nyingine ikiwemo rasimali watu na vitendea kazi vingine ili kazi iendelee kwa wakati huo ambao Katiba itakuwa imeelekeza uwepo wa Mahakama ya Juu,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile ametumia nafasi hiyo kuishukuru Mahakama kwa kukutana na wahariri huku akitumia nafasi hiyo kuwapingeza kwa mageuzi makubwa yanayoshuhudiwa katika mifumo na miundombinu.