Shirika la Umeme Nchini( TANESCO) limefanikiwa kupunguza makali ya Mgao wa Umeme kutoka wastani wa kati ya Megawati mia mbili(200) hadi mia mbili hamsini (250) wiki iliyopita hadi kufikia wastani wa kati ya megawati mia(100) hadi megawati mia hamsini (150) kutokana na kumalizika kwa matengenezo kwenye baadhi ya mitambo ambapo mtambo mmoja wa kituo cha kinyerezi namba || huku mtambo huo ukiwa umeanza kuzalisha Megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 24 November, kukamilika kwa mitambo miwili iliyopo katika kituo cha ubungo namba ||| ambapo unazalisha umeme wa megawati 35 hadi 40 kwenye Gridi ya Taifa imesaidia pia kupunguza changamoto za umeme.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tanesco Mhandisi Maharage Chande alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salam amesema kuwa jitihada zinazofanywa na shirika hilo kukabiliana na changamoto za upungufu wa Umeme nchini.
Aidha Mhandisi Chande ameongeza kwamba Mtambo mmoja wa Kidatu umeanza kufanya kazi na unazalisha Megawati hamsini(50) za umeme kwenye gridi ya Taifa, kukamilika kwa mitambo mingine miwili katika kituo cha upanuzi kinyerezi namba | imefanikiwa pia kuingia megawati 90 kwenye gridi ya Taifa.
Mhandisi Chande ameendelea kubainisha kuwa hali ya Ukame bado umesababisha mabwawa kupunguza ujazo wa maji hivyo uzalishaji wa umeme umekuwa wakusuasua akitolea mfano kituo cha New Pangani Falls ( NPF) kinazalisha megawati 7 pekee kwa sasa badala ya megawati 68.
Kituo Cha Hale kinazalisha megawati 4 badala ya megawati 10.5 , Kituo cha Kidatu kinazalisha megawati 145 kwa sasa badala ya megawati 204 na bwawa la nyumba ya Mungu megawati 4 badala ya megawati 8.
Aidha shirika hilo litaendelea kutoa taarifa za hali ya umeme pamoja na Ratiba za upungufu wa umeme kupitia ya www.tanesco.com.tz kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) katika magroup ya wateja wote nchini.