Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na uwekezaji Mh. Exaud Kigahe akitoa mwenendo wa bei za bidhaa hapa nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Uwekezaji TIC leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema ukame pamoja na kupanda kwa petrol kumesababisha kupanda kwa bidhaa za vyakula pamoja na vifaa vya Ujenzi
Akizungumza na waandishi wa habari leo Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na uwekezaji Mh. Exaud Kigahe Ametoa mwenendo wa bei za bidhaa hapa nchini ambapo amesema ukame pamoja na kupanda kwa Petrol kumesababisha kupanda kwa bidhaa za vyakula pamoja na vifaa vya Ujenzi.
Bei za bidhaa zimeendelea kutofautiana katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo sehemu nyingi bei za vyakula zimeendelea kupanda kutokana na kupungua kwa Uzalishaji katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021 hadi 2022 kutokana na hali ya hewa isiyoridhisha hapa nchini na nchi za jirani na kupanda kwa bei ya Petrol duniani.
Baadhi ya Mazao ya vyakula yaliyopanda bei Maharage, Viazi mviringo pamoja na mahindi.
Wizara ya viwanda Biashara na Uwekezaji kushirikiana na ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) zinashirikiana katika kukusanya takwimu katika masoko kuhusu bei ya mazao vyakula na vifaa vya Ujenzi kupitia maafisa masoko
Naibu Waziri Kigahe Amesema bei ya mahindi ya mwezi wa Desemba imefikia mia saba hamsini (750)hadi elfu moja mia nane Hamsini (1850) kwa kilo kulinganisha na mwezi uliopita ambapo mahindi yaliuzwa kwa mia saba(700) hadi elfu moja mia tano(1500) kwa kilo, baadhi ya mikoa ambapo ipo juu kwenye zao la mahindi ni Kilimanjaro, Mara na kigoma huku baadhi ya mikoa ambayo zao hilo lipo chini ni Iringa, Njombe, Songwe, na Ruvuma.
Aidha Unga wa ngano bei ni shilingi elfu mbili (2000) hadi elfu mbili mia tano(2500) Bei ya Sukari kwa mwezi huu wa Desemba ni shilingi elfu mbili mia sita(2600) hadi elfu tatu(3000) kwa kilo moja, Mafuta ya Alizeti bei ni shilingi elfu nne mia tano(4500) hadi elfu saba mia saba hamsini (7750) kwa lita moja huku mafuta ya mawese lita moja ikiwa ni shilingi elfu tano(5000) hadi elfu saba mia sita(7600).
Upande wa vifaa vya Ujenzi Saruji kwa mwezi huu wa Desemba unauzwa kwa elfu kumi na tano (15000) hadi elfu ishirini na nne(24000) kwa mfuko wa kilo hamsini (50) mikoa ambayo saruji ipo bei ya chini ni Tanga na Dar es salam huku mikoa ya Kagera, Kigoma na Katavi Bei ya Saruji ikiwa juu.
Kuhusu bei ya Nondo ni elfu kumi na mbili na mia sita(12600) hadi elfu ishirini na nane(28000) kwa nondo ya milimita kumi na mbili(12)huko mkoa ya Katavi, Iringa na Njombe bei ikiwa ipo juu na Mkoa wa Kilimanjaro na Dar es salam bei ikiwa chini.
Waziri Kihage amesema bidhaa za sabuni zipo kwa bei tafauti ambazo zinazalishwa hapa nchini ambapo kuna viwanda nane(8) vya kuzalisha Sabuni za maji na Vipande huku Sabuni nyingine zikiwa zinatengenezwa na viwanda vya wajasiriamali wadogo wadogo ambao wamepata wafunzo kutoka kwenye taasisi za Serikali kutoka Sido na Veta
Ameongeza kwamba lengo la Wizara ya Viwanda Biashara na uwekezaji kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa Bei za Bidhaa mbalimbali ili kuwawezesha Walaji, wadau pamoja na wazalishaji kujua taarifa sahihi za bei za Bidhaa ambazo wanatumia.