Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija akizungumza wakati akifungua Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu utaratibu wa matumizi ya mita za kukokotoa nauli za teksi za kawaida jijini Dar es salaam ambao umeratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini –LATRA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini –LATRA Johansen Kahatano akieleza faida ya Tax mita.
Wamiliki na madereva wa usafirishaji wa Tax kutoka katika maeneo mbalimbali mkoa wa Dar es salaam waliohudhuria katika Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu utaratibu wa matumizi ya mita za kukokotoa nauli za teksi za kawaida.
……………………
NA MUSSA KHALID
Wamiliki na madereva wa usafirishaji wa Tax mkoa wa Dar es salaam wametakiwa kutumia fursa ya kutoa maoni yao kuhusu utaratibu wa matumizi ya mita yatakayoiwezesha LATRA kwenda kutekeleza sheria ili kumuwezesha abiria anapoingia afahamu kiwango cha nauli anachopaswa kutoa.
Pia imeelezwa kuwa kwa kutumia Tax mita itasaidia abiria kutoa nauli ya kiwango kinachohitajika lakini pia itaongeza usalama kwa abiria hao kutokana na chombo hicho kutambulika kisheria.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija wakati akifungua Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu utaratibu wa matumizi ya mita za kukokotoa nauli za teksi za kawaida ambao umeratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini –LATRA.
Aidha DC Ludigija amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan imedhamiria kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha inakuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na kuongeza mapato pia kwa Taifa.
‘Nawapongeza sana LATRA kwa uamuzi wao kwani kila wakati wanapotaka kuanzisha au kutekeleza jambo jipya imekuwa ni kawaida yao kukutana na wadau kwa kuwapa elimu ili waweze kutoa maoni yao na waweze kuyafanyia kazi bila ya kuwa na manung’uniko’amesema DC Ludigija
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini –LATRA Johansen Kahatano amesema kuwa kuanzishwa kwa Tax Mita kutasaidia kuepukana na tax ambazo hazifati utaratibu wa usafririshaji.
‘Sisi LATRA tumekuwa tukipanga nauli kwenye vyombo tofauti hata UBA lakini leo hii hata ungepanga nauli abiria atajuaje hivyo ndo tukaamua kuja na chombo hichi kwa ajili ya kuwasaidia hawa watu wananchi pamoja na wasafirishaji wenyewe’amesema Kahatano
Kwa upande wao Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri wa huduma za Usafriri Ardhini-LATRA CCC Leo Ngowi ametoa mapendekezo kuhakikisha tax zote zinafungwa tax mita huku Mwenyekiti wa Tax mkoa wa Dar es salaam na Shirikisho la Tax Tanzania Ramadhani Hashiru amesema wameiomba LATRA kwanza kuboresha miundombinu.
Taxi Mita iligunduliwa na Mtaalamu Ujerumani Friedrick Wilhelim mwaka 1891 na baadae mwaka 1982 zikaboreshwa zaidi kuwa za kielektoniki na Afrika nchi 9 ndio zinatumia mfumo huo ikiwemo Egypt,Eritrea,Ghana,Morocco,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Afrika ya Kusini,Botswana,Nigeria pamoja na Rwanda.