Mtaalam wa Kinga na Udhibiti kutoka Jamii Bora, Said Chibwana akitoa mada katika semina ya wanahabari kuhusu ugonjwa wa Ebola iliyofanyika kwenye ukumbi wa Millenium Makumbusho jijini DAr es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya Bi. Catherine Sungura akifafaa jambo katika semina ya waandishi wa habari kuhusu ugonjwa wa Ebola semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Millenium Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
JAMII imetakiwa kuendeleza utamaduni wa kunawa mikono kwa usahihi ili kuondokana na magonjwa ya milipuko ikiwemo ebola.
Hayo yalibainishwa,Mratibu wa Kinga na Udhibiti magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokororo kwenye semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Wizara kwa ushirikiano na Mtandao wa Wataalam wa Afya wa Kiislamu (JAMII Bora) na USAID MTAPS
Alisema kuwa uko ushahidi wa kisayansi kuwa unawaji mikono sahihi una mchango mkubwa kupunguza kusambaa kwa magonjwa.
Dkt Hokororo alisema semina kwa wanahabari imelenga kuwapa uelewe ili waweze kuleta mabadiliko kwenye Jamii kupotoa unawaji mikono.
“Tumekutana Leo na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mkoa wa Dar es Salaam kuwajengea uwezo ili kupitia kakamu zao wakaielimishe jamii iweze kujikinga dhidi ya magonjwa ya milipuko hususani ugonjwa wa Ebola masuala ,”dkt Hokororo alisema.
“Tunaamini waandishi Wana mchango mkubwa kuibadilisha jamii kwahiyo wakiwa na uelewa wa kutosha watachochea mabadiliko kwenye jamii yetu kujikinga na maradhi haya,”aliongeza.
kwa Upande wake Mtaalam wa Kinga na Udhibiti kutoka Jamii Bora, Said Chibwana alisema unawaji mikono ulisaidia kudhibiti maambukizi kipindi Cha mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19.
“Tunaweza tukatumia uzoefu wa ugonjwa huo ili kukinga jamii dhidi ya ugonjwa wa Ebola ambao umesababisha vifo,”alisema Chibwana.
Aliongeza kuwa kwa kuhimiza jamii kuendeza Tania ya kunawa mikono itasaidia sana kupunguza na kumdhibiti maambukizi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ebola.
Naye Mshauri Mwandamizi kutoka Shirika la MSH Dr Doris Lutcam walofadhili mafunzo alisema lengo la mafunzo hayo kwa waandishi ni kuuelezea umuhimu wa jamii kuendeleza utamaduni wa kunawa mikono kila wakati ili kujiepusha na maradhi ya milipuko.