Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akikagua gwaride la kikosi maalum cha ulinzi wa maliasili katika kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati alipotembelea kijiji hichoukagua mradi wa uhifadhi wa msitu wa asili wa kijiji hicho hivi karibuni.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akizungumza na wanakikosi maalum cha kamati ya maliasili kijiji cha Malolo mara baada ya kukagua gwaride la kikosi hicho wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati alipotembelea kijiji hicho kukagua mradi wa uhifadhi wa msitu wa asili wa kijiji hicho hivi karibuni.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akikakipata maelezoktoka kwa kutoka kwa kiogozi wa kikosi maalum cha ulinzi wa maliasili katika kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa wakati alipotembelea kijiji hicho kukagua mradi wa uhifadhi wa msitu wa asili wa kijiji hicho hivi karibuni.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akikakipata maelezo kutoka kwa kutoka kwa mmoja wa walinzi wa kikosi maalum cha ulinzi wa maliasili katika kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati alipotembelea kijiji hicho kukagua mradi wa uhifadhi wa msitu wa asili wa kijiji hicho hivi karibuni.
Picha ya pamoja.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa uhifadhi wa msitu wa asili katika kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati alipotembelea kijiji hicho kukagua mradi wa huo hivi karibuni.
Kikosi cha ulinzi wa msitu waasilikatika kijii cha Malolo kikiwa kazini.
……………………………….
Jamii inayoshiriki katika usimamizi wa misitu imetakiwa kuwa mstari wa mbele kutekeleza vilivyo sera na sheria na taratibu zinazosimamia rasilimali za misitu ili kuongeza thamani ya maliasili hizo kwa manufaa ya taifa, jamii na wanavijiji wenyewe.
Afisa mawasiliano wa Mradi wa kuhifadhi misitu na kuwezesha Biashara endelevu ya Mazao ya Misitu Betty Luwuge kutoka Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa kuwahamasisha wanachi kuhifadhi misitu alipofanya ziara ya kukagua mradi huo katika kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa mkani Lindi hivi karibuni
Betty amesema kuwa engo la kufanya mradi huo ni kuongea na wadau wa Mradi na kuweza kushiriki na kuangalia matokeo chanya na namna wanaona mabadiliko tangu mradi huo uanze.
Aidha Betty amesema kuwa kutokana na ufadhili kukoma ndani ya Mwezi uiopita lakini Uhifadhi unaendelea kwani lengo lao ni kuhakikisha kwamba jamii inayoshiriki katika usimamizi wa misitu inakuwa mstari wa mbele katika kunufaika na kutekeleza sera na taratibu zinazosimamia misitu.
Amesema mradi huo mpaka Sasa wameweza kuwajengea uwezo wadau katika vijiji mbalimbali ikiwemo nyanja ya utawala Bora,Jinsi na jinsia, usimamizi wa rasilimali na kwenye Masuala ya sheria na namna wanaweza kusaidiana ili kuweza kuendeleza rasilimali Hizo.
“Kitu cha msingi ambacho tunaona kinahitaji kusimamiwa ni namna wananchi wanaendelea kusimamia rasilimali ikiwa kwa ni pamoja na kupata ushirikiano kutoka katika Halmashauri kuendelea kutambua misitu ambayo haijahifadhiwa Ili waweze kuisimamia”amesema Betty
Kuhusu faida inayotokana na misitu amesema ni kubwa hivyo amewasihi wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano Kwa kusimamia na kuwekeza katika eneo eneo Hilo.
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Malolo Abdala Said amesema Ili kuhakikisha wananchi wananufaika na uvunaji msitu katika kijiji hicho wanapewa elimu endelevu ambapo Wataalamu wamekuwa wakifanya utambuzi wa watu sambamba na uwezeshaji wa vikundi Ili kuweza kunufaika na mradi huo.
Amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza kufanyika kwa kuhakiki mipaka ya Kijiji na kuandaa mpango wa matumizi ardhi ya kijiji ambapo Jumla ya Hekta 1589 zilitengwa kuwa hifadhi ya msitu wa Kijiji na kati ya Hizo zilizotengwa kuwa Kijiji ni hekta 291.
Amesema kuwa Kijiji kwa Muda mfupi kimetekeleza mradi na kujipatia mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwezesha kutatua migogoro ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika kipindi kifupi.