****************

NA EMMANUEL  MBATILO

KLABU ya Simba imefanikiwa kuonoka na alama tatu mbele ya timu ya Polisi Tanzania baada ya kuichapa mabao 3-1 kwenye mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Ushirika mjini Moshi.

Kwenye mechi hiyo tumeshuhudia mshambuliaji wao Moses Phiri akiweka kambani  mabao mawili na kumfanya awe na mabao nane kwenye ligi kuu NBC na kuwa nafasi  ya pili kwenye ufungaji mabao huku akiongza Fiston Kalala  Mayele ambaye anamabao kumi.

Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco ambaye kwasasa amekuwa kwenye kiwango kizuri katika mechi tatu za hivi karibunu alivyoanza kupata nafasi kwenye kikosi.

Bao  pekee la Polisi Tanzania limefungwa na Zuberi Khamisi dakika za  lala salama