Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Mtwara kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Oktoba Mosi yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mtwara kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana, kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo na wa pili kushoto ni Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Mzee Seif Namtapika.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana akielezea ushiriki wa Wazee katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yatakayofanyika kitaifa Oktoba Mosi Mkoani Mtwara wa pili kulia ni Kamishna Wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo akielezea jinsi Serikali ilivyojipanga kuwahudumia Wazee nchini katika kikao na waandishi wa habari leo mkoani Mtwara kuhusu Maadhiishoya Siku ya Wazee Duniani Oktba Mosi yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mtwara.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.
*****************************************
Na Mwandishi Wetu Mtwara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yatakayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Manispaa ya Mtwara, Mkoani Mtwara.
Hayo yamesemwa leo mkoani humu na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi alipokuwa akitoa taarifa kuhusu Siku ya Wazee Duniani kwa niaba ya Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Kamishna Ng’ondi amesema kuwa Chimbuko la Siku ya Kimataifa ya Wazee ni tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa kupitia azimio Na. 45/106 la Mwaka 1990 ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisho siku ya Kimataifa Wazee kila ifikapo tarehe 01 Oktoba ya kila Mwaka.
“Lengo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki na mahijaji ya wazee. Kwa msingi huu, kupitia siku hii jamii hupata fursa ya kutafakari mafanikio, fursa na changamoto ili kuendelea kuboresha hali ya maisha ya Wazee” alisema Kamishna Ng’ondi.
Ameongeza kuwa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani hutoa fursa kwa wazee wenyewe, Serikali, Jamii, Vyama vya Siasa, Madhehebu ya dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuungana, kushiriki, kutafakari, kubainisha na kutatua changamoto zinazowakabili wazee katika utekelezaji wa maazimio, mikataba na matamko mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa yanayowawezesha wazee kuleta maendeleo yao na jamii nzima.
Ameitaja Kauli Mbiu kwa mwaka huu kuwa ni “Tuimarishe Usawa Kuelekea Maisha ya Uzeeni” ikiwa na lengo la kuhimiza nchi wanachama kuweka Mipango na mikakati ya kupunguza tofauti za watu katika jamii na kutoa fursa kwa makundi maalum kufaidika na fursa zilizopo na maendeleo yaliyofikiwa katika nchi husika.
Amesisitiza kuwa Serikali imejidhatiti katika kutoa huduma kww wazee ukizingatia ongezeko la idadai ya wazee duniani huku taarifa zinaonesha kuwa idadi ya Wazee duniani inaendelea kuongezeka. Kwa sasa wazee wanakadiriwa kufikia milioni 700 duniani. Idadi hii inatarajia kufikia bilioni 2 ifikapo kwama 2050 na kufanya asilimia 20 ya idadi ya watu wote duniani kuwa ni wazee. Aidha, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zitakuwa na ongezeko kubwa la wazee. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Tanzania inakadiriwa kuwa na Wazee 2,507,568 (Wanawake 1,307,358, Wanaume 1,200,210) sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.
“Ongezeko hili la idadi ya wazee ni kiashiria cha kuendelea kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma za msingi kwa jamii ikiwemo huduma ya afya ,upatikanaji wa chakula na huduma bora za matibabu; hivyo kuchangia kuongezeka kwa umri wa kuishi. Sote hatuna budi kujivunia na kuenzi mafanikio haya” alisisitiza Kamishna Ng’ondi.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Mtwara watatoa huduma za afya na Ustawi wa Jamii kwa wazee na wananchi wote wakakojitokeza katika madhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yakayoanza terehe 29 mwezi wa Tisa mpaka kilele Oktoba Mosi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muu gano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwjali wazee katika huduma za Afya na msamaha wa kodi za majengo ya makzi ila wameiombaSerikali kupeleke mswaada wa Sheria ya Wazee Bungeni ili kundi hilo litambulike kikamlifu