Ali Yahya Semwali mkazi wa kijiji cha Msolokelo kata ya Pemba wilayani Mvomero akizungumza na waandishi wa habari kuhusu unyanyasaji wa kijinsia katika kijiji hicho ambapo wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma kujadili mambo Mbalimbali kwenye Jamii.
Bi.Stamili Yusuf Kisingeli mkazi wa kijiji cha Msolokelo kata ya Pemba wilayani Mvomero akitoa ushuhuda wake juu ya masghirika ya TFCG na MJUMITA yalivyowakomboa wanawake kutoka kwenye unyanyasaji wa kijinsia.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akizungumza katika kikao hicho na wananchi wa kijiji cha Msolokelo.
Elida Fundi Afisa Sera na Majadiliano Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA akizungumza katika kijiji cha Msolokelo wakati wa ukaguzi wa miradi ya Mkaa Endelevu kijijini hapo.
Elida Fundi Afisa Sera na Majadiliano Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA kushoto, Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG wakiwa katika picha ya pamoja katika kijiji cha Msolokelo katikati ni Afisa misitu Wilaya ya Mvomero ndugu Edward Kimweri.
…………………………………………….
Imeelezwa kuwa elimu ya Jinsi na jinsia ambayo imetolewa kwa wananchi wa Tamaduni za Kinguu imesaidia kukabiliana na changamoto waliyokuwa wanakumbana nayo kwa wanawake wa kabila hiyo kutoonekana na thamani mbele za wanaume.
Hayo yameelezwa na Ali Yahya Semwali mkazi wa kijiji cha Msolokelokata ya Pemba wilayani Mvomero wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu (MJUMITA) walipofanya ziara kijijini hapo ambapo amesema kwa kipindi cha nyuma katika kijiji hicho wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma kujadili mambo Mbalimbali kwenye Jamii.
Amesema katika elimu ya Jinsi na jinsia imeweza kuwasaidia kuondoa ubaguzi na unyanyasaji kwa wanawake kuonekana kuwa hawana uwezo wa kufanya jambo lolote kwani hata kwenye mikutano na nafasi za uongozi wamekuwa wakishiriki.
“Wanawake walikuwa wanabanwa kwa kutoa kauli mbele za wanaume lakini baada ya Elimu hiyo kutolewa wamepata fursa ya kuzungumza popote”amesema
Amesema kuwa bado wanaendelea kuielimisha Jamii kuepukana na dhana zilizopo na wakati kwa kutowathamini badala yake waonyeshe Umoja na Ushirikiano kwao.
Mbali na hilo Semwali ameeleza mikakati mbalimbali wanayoifanya katika kuhifadhi misitu amesema katika Udhibiti wa misitu kupitia sheria walioelekezwa wamekaa na baadhi ya watu waliokuwa wanaharibu misitu na kuwapatia Mafunzo ya Uhifadhi.
“Hadi siku za nyuma zilizopita Kuna bwana Mmoja alivamia Kwenye msitu wetu wa hifadhi kwa ajili ya Kilimo na Kamati ya Maliasili walikwenda kule na kumkamata akapelekwa kituo Cha Polisi na alikiri kosa kisha alitozwa faini ya Tsh Laki Tatu”amesema Semwali
Aidha amesema kuwa baadhi ya waliokuwa wanaharibu misitu Kwa kuanzisha mashamba kwenye maeneo ya misitu wamekaa nao na kuzungumza nao jambo ambalo limesaidia kuyaacha na kuondoka.
Hata hivyo wanaendelea kuielimisha Jamii Ili kuhakikisha kuwa msitu inakuwa katika Hali ya Usalama wakati wote.
Naye Bi.Stamili Yusuf Kisingeli mkazi wa kijiji cha Msolokelo kata ya Pemba wilayani Mvomero ameshukuru kuja kwa mradi huo kwa sababu umemfanya kuwa mwanamke mwenye kujiamini kwa sababu alikuwa na Ng’ombe 3 lakini kupitia Mkaa Endelevu mpaka sasa ameongeza Ng’ombe kufikia 20, lakini pia amesomesha watoto wake mpaka kidato cha nne huku akishiriki katika vikundi mbalimbali vya kiuchumi.
Ameishukuru TFCG na MJUMITA kwa kuleta mradi huo kwakuwa umeawaondo wanawake kutoka kwenye lindi la umasikini na kuwafanya watu wenye uchumi mzuri.
Bi. Stamili ameongeza kuwa wanatamani mradi huu uendelee kwa sababu mpaka sasa hivi mazingira ni mazuri na wamefundishwa namna ya kuchoma mkaa endelevu huku miti ikikatwa kwa utaratibu wa utunzaji wa mazingira.