Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii Deosdedit Bwoyo wakati akizungumza na wanahabari kando ya mkutano kuhusu Warsha ya wadau wa Misitu Juu ya kujadili mikakati mbalimbali ya utafutaji wa fedha na kuwekeza katika misitu ya jamii na misitu mingine nchini Inayofanyika jijini Dodoma kwenye hoteli ya Morena.
………………………………..
Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa sera ya taifa ya misitu katika kipindi cha miaka 10 ijayo kuanzia 2021/2031.
Pia imeelezwa katika mpango mkakati huo imetengeneza mpango kazi wa usimamizi shirikishi wa misitu katika vijiji mbalimbali ili kuhakikisha inakuwa chini ya kijiji na kuhifadhiwa kisheria.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii Deosdedit Bwoyo wakati akizungumza na wanahabari kando ya mkutano kuhusu Warsha ya wadau wa Misitu Juu ya kujadili mikakati mbalimbali ya utafutaji wa fedha na kuwekeza katika misitu ya jamii na misitu mingine nchini ambapo amesema kuwa kila taasisi pamoja na wadau mbalimbali watakapotimiza wajibu wao misitu yote itakuwa vizuri.
Amesema kuwa licha ya Tanzania kubarikiwa kuwa na rasilimali kubwa za misitu takriban Hekta Mill 48.1 lakini kuna maeneo makubwa yanaanguka katika ardhi za vijiji na misitu hiyo ni michache ambayo tayari imeingia katika mpango wa usimamizi shirikishi.
Amesema kuwa kutokana na hilo Wizara imeanza hatua za kuhakikisha kuwa misitu inahifadhiwa kisheria kwa sababu ipi katika ardhi za vijiji ili kuepuka kuharibiwa.
Aidha Bwoyo amesema katika mkakati huo wanazihamasisha Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuangalia misitu sambamba na kujengewa uwezo wa kufahamu umuhimu wa misitu katika masuala ya kimaendeleo.
‘Tukifanya hivyo tunahamasisha hasa zile Halmashauri zenye rasilimali kubwa ya misitu ziweze kutenga fedha na kuandaa rasilimali watu katika kushiriki kwa ajili ya usimamizi wa misitu hiyo’amesema Bwoyo
Mkurugenzi huyo wa Misitu ameendelea kusisitiza kuwa uharibifu wa misitu inayopotea hauchangiwi na kitu kimoja bali ni pamoja na mambo mbalimbali yakiwemo ya uvunaji kiholela,kilimo cha kuhamahama na mifugo ambayo inaingizwa katika misitu.
Warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Morena jijini Dodoma imeandaliwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ushirikiano na Ofisi ya Idara ya Misitu na Nyuki ikifadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).
Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania MJUMITA, Rahima Njaidi akichangia mada katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa misitu uliofanyika jijini Dodoma kwenye hoteli ya Morena.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Morogoro Joseph Joachim Chuwa wakati akizungumza akiwasilisha mada katia warsha hiyo.
Bi. Crala Merchior Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uswiss akitoa shukurani zake kutokana na ushirikiano wa TFCG na ubbalozi huo kuhusu utunzaji wa misitu ya jamii ya vijiji.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG akiwa katika picha ya pamoja na na Austin Makani Muongozaji wa warsha hiyo.
Picha mbalimbali zikiwaonesha washiriki wa warsha hiyo ya wadau wa misitu iliyofanyka kwenye hoteli ya Morena jijini Dodoma leo.
Picha ya pamoja.