Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo makamishna/wajumbe wapya na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC).
Mafunzo hayo yanahusisha wajumbe wapya wa Tume za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambazo ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lethoto, Malawi na Tanzania na yameanza leo Novemba 22 hadi 25 ,2022 jijini Dar es Salaam. (Picha na NEC).