Picha mbalimbali za uchaguzi mkuu wa CCM mkoani Pwani
…………………
Novemba 22
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoani Pwani ,Mwinshehe Mlao amewaonya wenye magomvi ndani ya mkoa huo waanze kupatana, ama kupatanishwa kwani magomvi hayana nafasi kwenye uongozi wake.
Aidha, amejipanga kuhakikisha anamaliza miradi ya kiuchumi iliyoanzishwa ndani ya Chama na kuanzisha miradi mipya itakayoinua uchumi wa Chama mkoa.
Akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa wa Pwani ,baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata kura 471 ,Mlao alieleza yeye sio muumini wa magomvi kwani yanadidimiza maendeleo na hayaleti mshikamano.
Alifafanua, kwasasa mkoa haupo vizuri,kuna makundi ndani ya wilaya ,hivyo atahakikisha anasimamia ushirikiano na mahusiano ili kuimarisha Chama hicho.
“Tuungane tuwe pamoja kusaka ushindi wa CCM 2025 , Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu ndio kiongozi wetu kila siku anahimiza umoja,tusibaki nyuma kwa ubinafsi wetu, miezi minne iliyopita nilisikia mkoa wetu haupo katika Hali nzuri ,wakati nakabidhi kijiti huko nyuma niliacha mkoa tukiwa wa Saba katika kumi bora”
“Hatuwezi kuharibu Chama Cha watu kinachoaminiwa kwa sababu ya magomvi ya wachache,Naomba mpatane mlio kwenye magomvi ,kama hamwezi tafuteni wa kuwapatanisha “jambo la ugomvi halina dharura,mnakuwa mmekusudia haswaaa, mkikosa wa kuwapatanisha Mimi na wenzangu tutaangalia namna ya kuchukua hatua kwa kufuata Utaratibu na kanuni za Chama ili kukomesha tabia hiyo”
“Niliwahi kusikia watu wanasema Mlao mkali,hapendi watu ,hapana!!,nataka tuungane tukiacha Chama tuache katika mikono salama ,Lazima tuambizane ukweli na mambo yatakayosaidia Chama chetu “alibainisha Mlao.
Awali msimamizi wa uchaguzi wa CCM Mkoani Pwani, Zainab Telaki alitangaza Mlao alishinda kwa kupata kura 479 dhidi ya mgombea wa pili Farida Mgomi aliyepata kura 341.
Alifafanua, Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti ulirudiwa ambapo wajumbe walitakiwa kuwa 824, kura ziliharibika 4 halali zilipigwa kura 820.