Gari likitoa mosho.
Muonekano wa vituo vya ukaguzi wa magari na vyombo vingine vya moto.Vituo vya ukaguzi wa magari na pikipiki.
Dar es Salaam.
KUFUATIA ziara iliyofanywa nchini Misri na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni imeanza kuonesha matunda ambapo baadhi ya wawekezaji kadhaa ikiwepo Kampuni ya Kimataifa ya GS Investment Group yenye makao makuu yake Cairo Egypt nchini humo kuonesha nia ya kuwekeza katika eneo la mazingira.
Akizungumza kwa njia ya simu Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo (CEO) Gasser El-Sayed ambaye anaiendesha yenye mapato ya dola za kimarekani billion mbili (2 billion USD ) kwa mwaka ameonesha nia ya kuwekeza katika eneo la VEHICLE INSPECTION CENTERS na TRAFFIC Management Solutions kwenye mikoa yote Tanzania kwa njia ya PPP.
El-Sayed alisema kwa sasa wameanza kufuatilia vibali, utaratibu na kanuni zote za uwekezaji kutoka Serikalini kabla ya kuanza Uwekezaji huo nchini.
“Baada ya ziara ya COP27 ya Rais wa Tanzania Egypt, tumeona ni fursa njema kuleta uwekezaji wetu Tanzania kama tulivyofanya Ghana, Chad, Nigeria, Dubai na Saudi Arabia, na tumekusudia kuja kuwekeza kwenye eneo la VEHICLE INSPECTION CENTERS na tutajikita zaidi katika masuala ya usalama barabarani ambapo tutatumia mageuzi ya kidigitali katika kufanya shughuli hiyo” alisema.
El-Sayed alisema mazingira ya mradi huo utaisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchi kama Ilivyokuwa kwenye nchi nyingine ambapo Mapato yaliongezeka kwa asilimia 60% baada ya uwekezaji wao.
Alisema katika kutekeleza suala hilo watajenga mitambo maalumu Nchi Nzima ambazo zitatumika kukagua magari yote na vyombo vingine vya moto kama pikipiki ambavyo vitakuwa havina ubora, kama kutoa moshi na uchakavu na kuhakikisha Usalama wa barabarani.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika na imekuwa ikijishughulisha kutengeneza mbolea, masuala ya afya, bidhaa za ngozi, na kwa sasa wana mkataba wa kutengeza Pia Vifaa Vyote vinavyotumika kwenye World Cup Qatar na FIFA ikiwemo mipira na mambo mengine mbalimbali.
Alisema tayari kampuni hiyo imekuwa ikifanya majadiliano na Serikali kwa takribani Mwaka na nusu sasa na wana imani michakato iko kwenye hatua za mwisho kuhusu masuala na maeneo ambayo serikali itapendekeza kufanya.
Alisisitiza kuwa uwekezaji huo kwa awamu ya kwanza wataanza na kazi hiyo na baadae iwapo watakubaliwa wataingia katika masuala mengine ikiwemo kujenga viwanda na mifumo mbalimbali ya kuweza kusaidia Serikali kwenye ukusanyaji wa mapato.