Alex Sonna-DODOMA
SPIKA Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai aliibua shangwe baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi Chama Cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Dodoma kumpendekeza kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa uchaguzi na kukubali ombi hilo.
Wakimshangilia kwa makofi na vigelegele Ndugai ambaye alikuwa amekaa walipokuwa wajumbe aliinuka na kwenda meza kuu.
“Ninashukuru kwa heshima hii , asanteni wajumbe kwa kuniamini” álisema.
Kabla ya wajumbe kumpendekeza Ndugai, Mkutano huo ulikuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa ambaye alijiuzulu nafasi hiyo kutokana na kuwa mgombea anayetetea nafasi yake ya Uenyekiti.
Nafasi ambazo zinapigiwa kura na wajumbe hao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma ,Mjumbe wa Halmashauri kuu NEC Mkoa na Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM mkoa wa Dodoma.