Diwani wa kata ya Matuli na Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ndugu Lucas Lemomo akizungumza mbele ya maofisa wa mashirika ya TFCG na MJUMITA hawapo pichani walipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Matuli kwenye vijiji vya Diguzi, Lulongwe na Mlilingwa mkoani Morogoro Novemba 20,2022.
…………………………..
Mradi wa mkaa Endelevu ambao unaosimamiwa na shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA umekuwa faraja na chachu ya maendeleo katika jamii na vijiji ambapo umeleta faida kubwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea miradi mbalimbali kama vile Ujenzi wa Zahanati katika Vijiji vya Diguzi, Lulongwe na Mlilingwa mkoani Mororgoro pamoja na ukarabati wa maradasa, ujenzi wa vyoo vya shule, Zahanati na kuwakwamu wananchi kiuchumi.
Hii inatokana na uelewa ambao wananchi wameupata juu ya namna bora ya uvunaji wa misitu kupita mradi wa Mkaa Endelevu kwa njia za kisasa na utunzaji wa misitu ya asili katika vijiji vyao.
Hayo yameelezwa na Diwani wa kata ya Matuli na Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ndugu Lucas Lemomo alipokuwa akizungumza mbele ya maofisa wa mashirika hayo walipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Matuli kwenye vijiji vya Diguzi, Lulongwe na Mlilingwa
Bw. Lucas Lemomo amesema baada ya mradi wa mkaa Endelevu kufika katika vijiji vya Diguzi, Lulongwe na Mlilingwa wananci wa vijiji hivyo na vitongoji vyake wamefaidika na mambo mengi ikiwemo kupata elimu ya masuala mbalimbali kama vile mambo ya utawala bora, mafunzo ya kijinsia , mafunzo ya uvuna mkaa endelevu na utunzaji wa misitu, Kilimo na masuala ya fedha kama vile uanzishwaji wa vikundi vya Saccos jambo ambalo limesaidia wananchi kupata uelewa wa mambo mbalimbali na kujiendeleza kiuchumi lakini pia vijiji vyao kutekeleza miradi ya maendeleo kutokana na uvunaji wa mkaa endelevu.
“Kijiji cha Lulongwe tayari kimeshapata ufadhili wa ofisi ambapo kabla ya hapo walikuwa wanakaa chini ya miti lakini baada ya mradi huu wa Mkaa Endelevu kuanza wamepata ofisi ambayo sasa wanaitumia,” Amesema Lucas Lemomo
Ameongeza kuwa pia wameweza kufanya matumizi bora ya ardhi wananchi wote wana hati za viwanja na mashamba, ambapo zimetolewa hati za kimila zinazowamilikisha ardhi kwa miaka yao yote na wanaweza kuwarithisha watoto na wajukuu wao.
Serikali kupitia Wizara wameleta umiliki ardhi wa ambapo wanamiliki viwanja lakini kwenye mradi wa mkaa Endelevu wananchi wanapata elimu namna bora ya kulinda misitu, wananchi wanatumia asilimia kumi (10) tu ya misitu na asilimia tisini (90) wanailinda ambapo asilimia 10 imepagwa kutumia ndani ya miaka ishirini na nne (24).
Akizungumza kijiji cha Diguzi amesema kijiji hicho kimeweza kukusanya zaidi ya milioni 80 kupitia mkaa endelevu ambazo zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo na hizo ni fedha za ndani ya kijiji huku kijiji cha Matuli zikipatikana kiasi cha shilingi miloni 104 ambazo wametumia katika kujenga vyoo vya shule, Zahanati pamoja na madarasa jambo ambalo limesaidia vijiji hivi kupata maendeleo
Ameongeza kuwa Kijiji cha Lulogwe kimeweza kukusanya fedha nyingi ambapo kiasi cha shilingi milion tano(5) zmekarabati madarasa, wamekarabati nyumba mbili za walimu kwa shilingi milioni(50) kupitia mradi wa mkaa Endelevu pia wamejenga kituo cha Afya ambacho kimegharimu shilingi milioni (150) huku milion hamsini zikitoka kwenye serikali kuu.
Kuhusu matumizi bora ya ardhi amesema kwamba wananchi wa kijiji hicho wanazingatia matumizi bora ya ardhi huku ulinzi wa misitu ukiwa unaendelea, sasa hivi wananchi wameshapata elimu namna bora ya kulinda misitu, huku akieleza kwamba hakuna tena uvunaji usiofuata utaratibu.
“Zamani ukipita katika barabara nyingi za vijiji utakutana na wananchi wakiwa wamebeba magunia ya mkaa lakini kutokana na elimu ambayo imetolewa na TFCG na MJUMITA kwa wananchi kila mwananchi ni mlinzi wa misitu kwa sababu wanajua misitu ikivunwa hovyo hawatapata faida pamoja maendeleo katika vijiji vyao,” Amesema Bw. Lucas Lemomo.
Ameishukuru TFCG na MJUMITA kwa kutoa elimu hiyo kwa wananchi , imewapa uelewa wa namna bora ya kulinda misitu hasa ukizingatia kuwa mradi huo wa mkaa Endelevu unaenda kufikia ukomo wa utekelezaji wake, lakini wananchi watabaki na elimu ya utunzaji wa misitu hivyo wataendelea kuvuna mkaa kwa njia ya kisasa kwa sababu tayari elimu ya utunzaji wa misitu wanayo.
Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya jamiii(USMJ) ulikuwa unatekelezwa chini ya Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya Misitu (CoForEST) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).
Elida Fundi Afisa Sera na Majadiliano Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA akizungumza katika kijiji cha Lulongwe wakati alipotembelea kijiji hichokukagua utekelezaji wa miradi kushoto ni Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge.
Diwani wa kata ya Matuli na Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ndugu Lucas Lemomo na Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge wakipata maelezo ya mradi wa zahanati ya kijiji cha Lulongwe.
Muonekano wa jengo la Zahanati ya Lulongwe ambayo imejengwa na kijiji kwa mapato ya fedha za mradi wa mkaa Endelevu na serikali kuu
Diwani wa kata ya Matuli na Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ndugu Lucas Lemomo na Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge wakikagua nyumba ya walimu katika kijiji cha Lulongwe.
Bi Zainab Athman akionesha nyumba yake ambayo anaijenga kwa mapato ya fedha za mradi wa Mkaa Endelevu katika kijiji cha Mlilingwa.