Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera (kushoto ) akisalimiana na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kufunga Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu). Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera akipiga mpira wa gofu ikiwa ishara ya kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu). Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera (kulia ) Balozi wa Tanzania Malawi Mh Humphrey Polepole (Katikati ) na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu).
*************************
Na Meja Selemani Semunyu MALAWI
Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera ameishukuru Tanzania kupitia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda kwa ushirikiano inaouonyesha kwa nchi hiyo na jeshi lake kupitia michezo ikiwemo Gofu.
Rais Chakwera aliyazungumza hayo wakati wa sherehe za ufungaji wa mashindano ya gofu ya kuwaenzi na kuwachangia maveterani wa vita yaliyofanyika katika Uwanja wa Gofu wa Lilongwe nchini Malawi.
“ Ninanawashuru Ndugu zetu kutoka Tanzania hakuna nchi ambayo haipati Changamoto za kiuchumi na hakuna Nchi ambayo haipambani kutatua shinda za wananchi wake na mahitaji yao lakini kikubwa ni kusaidiana na Kuchangiana kufanikisha hilo “ Alisema Rais Nundwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi wa Malawi Jenerali Vicent Nundwe alisema ni heshma kubwa kwa jeshi lao kupata ugeni huo ambao umezidi kuongeza ushirikiano.
“ Najua mmesafiri kutoka Mbali kuja Malawi hii ni heshima kubwa kwetu tunawashukuru sana kwa kuacha shughuli zenu na kuja kutuunga mkono katika Mashindano haya.” Alisema Jenerali Nundwe.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mh Humphrey Polepole alisema kama Ubalozi wanamshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda kwa kuruhusu utekelezwaji wa Diplomasia kupita Michezo.