Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Nishati Kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia sera za nishati mbadala ili kufikia malengo ya serikali yakutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2032
Raisi Samia ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati wa akifunguzi wa mjadala wa kitaifa wa siku mbili wa kujadili matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi ya nishati chafu.
Hata hivyo amesema kuwa kikosi kazi hicho kitaongozwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na kitahusisha Wizara mbalimbali zinazohisika katika utunzaji wa mazingira ikiwemo Wizara ya Nishati, TAMISEMI,Wizara ya Muungano na Mazingira ,Wizara ya Afya,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake,Ofisi ya waziri mkuu,sera,bunge na uratibu na Makundi Maalumu pamoja na sekta binafsi..
“Nimetoa pendekezo la kuunda kikosi kazi cha kuangalia kuhusu kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia. Bajeti ijayo tutakwenda kutenga fedha ya kutosha kwa ajili ya mfuko wa nishati safi ya kupikia.” amesema Rais
RAIS amesema kuwa kikosi hicho kitakua na kazi kubwa ya kuchakata sera nakuja na afua zitakazosaidia kuandaa sera na sheria zitakazowezesha kusimamia matumizi nishati safi,salama na endelevu ya kupikia ,ambapo amebainisha kuwa kufikia mwaka 2032 angalau asilimia 80 hadi 90 ya watanzania wawe wanatumia nishati mbadala nakuondokana na madhara yatokanayo na matumizi ya nishati chafu yakiwemo mkaa,kuni ambapo Ina madhara ya kiafya na kimazingira .
Rais Samia amesema serikali katika mwaka wa fedha 2023 / 2024 inatarajia kutenga fedha ya kutunisha mfuko wa nishati safi ili kuweza kuwa na rasilimari fedha kwa ajili ya kuwezesha watanzania waishio kwenye mazingira magumu hasa vijijini waweze kutumia nishati safi nakuachana na utumiaji wa mkaa na kuni ambao umekuwa ukisababisha kupungua kwa misitu na kutokea mabadiliko ya hali ya hewa ilkiwemo ukame .
“Hali ya upungufu wa maji katika Mikoa mingi hasa,Morogoro,Iringa,Pwani huku Mkoa wa Dar es salaam kukiwa ma mgao wa maji hali hii inatokana na shughuli za binadamu ikiwemo ukataji miti holela pasipo kupanda hivyo vyanzo vya maji kupungua maji suala Hilo lazima liangaliwe kwa jicho la tatu la sivyo madhara yanaweza yakawa makubwa isipodhibitiwa mapema”amesema Rais
Kwa upande wake Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema nishati ya kupikia inatumika kila nyumba huku nishati ya mkaa ikiwa ikitimika sana hivyo suala hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wake nakuweza kufikia malengo ya serikali yakuondoa changamoto za gharama zitokanazo na matumizi ya nishati chafu.
“Mheshiniwa rais nishati safi inaweza kubadilisha maisha ya watanzania kutokana na matuzmizi safi,kupika huku unatoa machozi,kamasi ,unakohoa sio jambo zuri ,kupika ni furaha ,hivyo matumizi ya nishati safi tutaokoa afya za watanzania,pia watoto wanaoshindwa kufikia ndoto zao kielemu kutokana na kazi za kutafuta kuni.” alisema Makamba.
Nae Profesa Tubaijuka ameishauri serikali kuhakikisha inangalia namna ya kupunguza gharama ya gesi ,ambapo kadri miaka inavyozidi kusogea imekuwa ikipanda kutoka bei ya awali 18000 nakufikia 24000 hali ambayo kwa mtanzania wa maisha ya kawaida hawezi kumudu gharama hizo.
Aidha Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili ,Dkt. Pauline Chale alisema kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ikimekua ikihudumia 60 kwa siku ambapo miongoni mwao ni wale waliopatwa na madhara ya nishati chafu hivyo elimu ya kubadilisha mtazamo wa watanzania kuacha kutumia nishati chafu inahitajika kwa haraka.
Mkutano huo wa utakuwa siku mbili umewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ,pamoja na taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, ikiwa lengo ni kujadili namna yakutoka katika matumizi ya nishati chafu nakuhamia katika matumizi ya nishati Safi,Salama na Endelevu.