Bw. Emmanuel Mabisa mratibu wa Tamasha la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na nchi Kwa ujumla litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Akuzungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Msama Promotion Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi ya Tamasha Hilo ambapo amesema waimbaji mbalimbali watashiriki Julia ni Rose Muhando mwimbaji wa nyimbo za injili.
Bw. Emmanuel Mabisa mratibu wa Tamasha la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na nchi Kwa ujumla litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Akimsikiliza mwibanji nyimbo za injili Rose Muhando wakati akitoa ratiba ya matamashs mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za Msama Promotion Kinondoni jijini Dar es Salaam
Maandalizi ya Tamasha la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na taifa ambalo litafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika Kwa asilimia mia moja.
Hayo yameelezwa na mratibu wa Tamasha Hilo Kutoka Kampuni ya Msama Promotion Bw.Emmanuel Mabisa wakati akizungumzia Maandalizi hayo kwenye ofisi za Kampuni hiyo Kinondoni jijini Dar es Salaam Leo Novemba 02,2022.
Amewasihi watu mbalimbali kujitokeza Katika Tamasha Hilo ambalo kiingilio kitakuwa shilingi 2000 Kwa wakubwa na Kwa watoto shilingi 1000.
Ameongeza kwamba maaskofu na wachungaji mbalimbali watafanya maombi kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na taifa Kwa ujumla ili aweze kuendelea kutenda kazi yake ya kuliongoza taifa Kwa hekima kubwa na baraka tele Kutoka Kwa mungu wakiwemo waimbaji Kutoka mataifa mbalimbali kama vile Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania yenyewe.
Kwa upande wake mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando amethibitisha kushiriki Katika Tamasha Hilo na kueleza kuwa Yuko tayari kushiriki Katika kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anapambana sana Katika kuiletea nchi Maendeleo na amethubutu hata kuvaa uhusika kama mama wa familia ambaye amekuwa akipambana huku na kule kutafuta ili watanzania tuweze kupata Maendeleo Katika nchi yetu.
Amesema Katika nchi zetu za Afrika Mashariki Marais wote ni wanaume lakini Rais pekee mwanamke ni Mh.Samia Suluhu Hassan ametuheshimisha sana kama watanzania.
Tuna Kila sababu ya kumnyanyua kumshika mkono na kutembea Naye kifua mnele ili aweze kubarikiwa na kufanya kazi ya kuliongoza taifa hili Kwa Nguvu za mungu Kwa sababu mwanamke ni mama ni kiongozi wa familia na mlezi pia watanzania tunampenda Kwa sababu ni wa kwetu hakuna mwingine wa kumpenda zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan tuliyepewa na mungu mwenyewe.
Rose Muhando ametaja mikoa mingine ambayo Tamasha Hilo litafanyika kuwa ni Dodoma, Dar es salaam, Mbeya pamoja na Arusha.