Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi, Bw. Nahson Sigalla akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wakati wa kikao cha kukusanya maoni kuhusu nauli mpya za MV. NJOMBE, MV. MBEYA II na MV. RUVUMA
Bi.Eugenia P Punjila, Afisa Masoko Mkuu kutoka MSCL akitoa ufafanuzi kuhusu nauli mpya za meli za MV. NJOMBE, MV. MBEYA II na MV. RUVUMA
Baadhi ya wadau waliofika kutoa maoni kuhusu nauli mpya katika Wilaya ya Kyela
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi, Bw. Nahson Sigalla akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wakati wa kikao cha kukusanya maoni kuhusu nauli mpya za MV. NJOMBE, MV. MBEYA II na MV. RUVUMA
TASAC, MSCL wakusanya maoni ya wadau nauli mpyaShirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeahidi kufanyia kazi mapendekezo ya wadau wa usafiri kwa njia ya maji kuhusiana na nauli mpya za meli ya MV. Njombe, Mv. Mbeya II na MV. Ruvuma zilizopendekezwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kukusanya maoni ya wadau katika Ukumbi wa Mji mdogo Kyela,
Mkurugenzi wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amesema TASAC imeamua kufanya kikao hicho baada ya kupokea maombi kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) juu ya viwango vipya vya nauli za abiria na ubebaji wa mizigo kwa safari za meli za Mv. Njombe, Mv. Mbeya II na Mv. Ruvuma zinazofanya safari katika Ziwa Nyasa.
“Kampuni ya MSCL ilikabidhiwa meli hizi 3 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) hivyo kwa sasa ndiyo mwendeshaji wa meli hizi, imewasilisha maombi ya mapitio ya nauli zitakazotumika kwa abiria na mizigo kwa kuzingatia gharama za uendeshaji ili kuiwezesha Kampuni kuendelea na jukumu lake la kutoa huduma za usafiri katika Ziwa Nyasa” amesema Mkeyenge.
Aidha aliongeza kuwa, kwa mujibu wa sheria TASAC ina jukumu la kuratibu Mkutano huu wa wadau wa huduma ya usafiri majini ili kukusanya maoni kuhusu viwango vya nauli vilivyopendekezwa na MSCL.
“Katika Mkutano wa leo tutapokea maoni ya wadau hivyo nitoe wito kwa wadau waliopo hapa kutoa maoni katika Mkutano huu na hata baada ya huu TASAC itaendelea kupokea maoni kwa maandishi, ikiwemo barua, hadi tarehe 14 Novemba, 2022” amesemaM keyenge.
Naye Bi. Eugenia P Punjila, Afisa Masoko Mkuu wa MSCL mabadiliko ya nauli yametokana na gharama za uendeshaji kupanda ukizingatia meli ni mpya na matumizi yake yako juu.
Aidha aliongeza kuwa, mapato yanayotokana na meli hizo ndio yatakayotumika kuhudumia ukarabati wa meli hizo, gharama za mafuta, chakula cha watumishi wa meli hizo wawapo safarini pamoja na mishahara ya watumishi.
Kwa upande wa wadau walioshiriki katika kikao hicho wameomba nauli zilizowekwa zipunguzwe ikizingatiwa hali duni ya uchumi wa watumiaji wa usafiri huo.
TASAC kwa kushirikiana na MSCL wameanza kukusanya maoni ya wadau kuhusu nauli mpya katika maeneo ya Kyela, Manda na Mbaba Bay.