Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dkt. akizungumza na waandishi WA habari Katika semina ya Utabiri WA Hali ya Hewa ambapo pia alitoa vyeti Kwa waandishi Bora wa habari za Hali ya Hewa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dkt. Dkt. Buruhani Nyenzi akitoa cheti Kwa mwandishi Bora wa jumla wa habari za Hali ya Hewa Irene Marck Kutoka Jamvi la Habari Katika semina ya Utabiri wa Hali ya Hewa iliyofanyika kwenye hoteli ya Tiffany Diamond Hotel jijini Dar es Salaam, Katikati ni Mwandishi mbobezi wa habari za Hali ya Hewa Bw. Mbaraka Islam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dkt. Dkt. Buruhani Nyenzi akitoa cheti Kwa mwandishi Bora wa habari za Hali ya Hewa kipengele Cha Electronic Mussa Khalid Kutoka Kiss FM Katika semina ya Utabiri wa Hali ya Hewa iliyofanyika kwenye hoteli ya Tiffany Diamond Hotel jijini Dar es Salaam , Katikati ni Mwandishi mbobezi wa habari za Hali ya Hewa Bw. Mbaraka Islam.
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt Hamza Kabelwa akizungumza Katika semina hiyo wakati alipotoa mada kuhusu waandishi wa habari kuwa mabalozi wazuri wa Habari za Utabiri wa Hali ya Hewa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa Katika semina hiyo.
……………………………
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini -TMA imewasihi wanahabari kuendelea kuwa mabalozi wa kutoa taarifa za Hali ya Hewa kwa usahihi ili wananchi waweze kupata taarifa hizo kwa ukamilifu.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt Hamza Kabelwa wakati akifungua warsha ya wanahabari kuhusu muelekeo wa msimu wa mvua kipindi cha Mwezi Novemba 2022 mpaka April Mwaka 2023 sambamba na kutoa tuzo kwa wanahabari waliofanya vizuri Katika kutoa taarifa za Hali ya Hewa.
Amesema kupatikana kwa Utabiri huo kwa usahihi na kwa wakati utachangia katika jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na nchini kwa ujumla.
“Kwa Mwaka wa pili sasa mfulululizo Mifumo ya Hali ya Hewa kwa Mwaka huu pia inaashiria upungufu wa Mvua matika maeneo yanayopata Mvua za msimu hivyo nawaomba wanahabari kufikisha taarifa hii kwa usahihi”amesema Hamza
Aidha Dkt Hamza amesema taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na athari zake ni muhimu kupatikana kwa wakati ili kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
Dkt Hamza amesema kuwa TMA inamchango mkubwa katika ukuaji wa kiuchumi kwa vile huduma za hali ya hewa ni mtambuka na zinahitajika katika kila sekta.
Vilevile amewataka wanahabari kuhakikisha wanafuatilia taarifa za hali ya hewa za kila siku ikiwa ni pamoja na za hali mbaya ya hewa zinapata nafasi katika vyombo vyao vya habari ili wananchi waweze kunufaika na taasisi hiyo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.