Mkurugenzi Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sadati Musa, akimkabidhi tuzo ya ngazi ya juu ya uanachama (TIOB Fellowship), Afisa Mkuu wa Udhibiti wa Benki ya NMB, Doreen Joseph, iliyotolewa na Taasisi ya Wataalamu wa Kibenki (TIOB) kwa wanachama wake. hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo Dk. Charles Kimei, akimpongeza Afisa Mkuu wa Udhibiti Benki ya NMB, Doreen Joseph baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna.
Afisa Mkuu wa Udhibiti Benki ya NMB, Doreen Joseph, akiwa ameshika tuzo ya ngazi ya juu ya uanachama iliyotolewa na Taasisi ya Wataalamu wa Kibenki (TIOB) kwa wanachama wake. hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Doreen alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB.