Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jaffo (katikati), akipanda mmoja ya miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na (kushoto) ni Afisa Tawala Wilaya Magamoyo mkoani humo, Casilda Mgeni, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jaffo na (katikati) Afisa Tawala Wilaya Magamoyo mkoani humo, Casilda Mgeni wakishuhudia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Bw. Helman Kasekende akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jaffo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Bw. Helman Kasekende wakiongozana kwa ajili ya zoezi la kupanda miti katika shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Bw. Helman Kasekende akizungumza katika hafla hiyo ya upandaji wa miti iliyofanyika kwenye shule ya msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Picha mbalimbali zikiwaonesha wadau mbalimbali walioshiriki katika zoezi hilo la upandaji wa miti katika shule ya msingi Mtoni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benkiya Standard Chartered, Herman Kasekende kushoto ni Afisa Tawala Wilaya Magamoyo mkoani humo, Casilda Mgeni.
……………………………………..
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani Jafo ameipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kuamua kupanda miti katika Shule ya Msingi Mtoni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani huku akiziomba taasisi za serikali na binafsi nchini kuiga mfano wa Benki hiyo.
Dkt. Jafo ameyasema hayo baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule hiyo wilayani Bagamoyo ambapo amewahimiza wananchi kuendelea kuhamasishana kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza mazingira.
Aidha amesema ajenda ya mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara huku akiwataka wanafunzi kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki katika zoezi zima la kupanda Miti katika maeneo yao.
“Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi miongooni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali na binafsi nchini,”amesema Dkt. Jafo
Ametanabaisha kuwa ni vema suala la upandaji miti katika nchi yetu liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira jambo ambalo litaokoa mazingira na kulifanya taifa kuepukana na uharibifu wa mazingira na ukame.
Ameongeza kuwa upandaji wa miti kwa wingi kwenye mazingira ni njia moja wapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadamu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende amesema amefarijika sana kuona watanzania wanapanda miti kwa wingi.
“Nitaendelea kuunga mkono juhudi mbalimba na kuhakikisha Tanzania inakua ya kijani kama maelekezo ya serikari ya kupanda miti katika maeneo yote nchi nzima inavyoelekeza.” Amesema Bw. Helman Kasekende.