Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (katikati) Prof. Lawrence Museru akiwa na baadhi ya viongozi wa Muhimbili pamoja na viongozi kutoka Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) wakijadiliana juu ya hati ya makubalino kati ya KOFIN na Muhimbili.
Prof. Museru akipitia hati ya makubaliano ambayo itasainiwa kesho.
Bi. Kim Hyunkyong kutoka KOFIH akifafanua jambo kuhusu uboreshaji wa huduma za afya.
Baadhi ya viongozi wa MNH wakiwa kaika picha ya pamoja na viongozi kutoka KOFIH mara baada ya kumaliza majadiliano yaliyofanyika leo Muhimbili-Mloganzila.
…………………..
Dar es salaam
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo umekutana na uongozi kutoka Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) kwa lengo la kupitia na kujadiliana juu ya hati ya makubaliano kati ya KOFIH na MNH ili kuimarisha masuala ya uongozi wa hospitali pamoja na kuwajengea uwezo watumishi katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla.
Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema makubaliano hayo yatahusisha wataalam kutoka Korea kuja Tanzania ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa watalaam wa Hospitali ya Mloganzila.
Kupitia makubaliano hayo wataalam wa Mloganzila watapata fursa kwenda nchini Korea kwa ajili ya kupata mafunzo ya fani mbalimbali za huduma ya afya.
“Wataalam kutoka Korea tumekua tukishirikiana nao katika kutoa huduma za afya ikiwemo za kibingwa na hatua hii ni fursa nzuri kwa wataalam wazalendo kuendelea kujengewa uwezo zaidi na kubadilishana uzoefu” amesema Prof. Museru.
Hati ya makubaliano (Memorandum of Understanding) inatarajiwa kusainiwa kesho.