Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana akizungumza wakati akizindua Bodi ya wakurugenzi Makumbusho ya Taifa katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Oswald Masebo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi Makumbusho ya Taifa katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi Makumbusho ya Taifa katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugezi wa Idara ya Malikale Dkt Emmanuel Bwasili akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi Makumbusho ya Taifa katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi Makumbusho ya Taifa.
Picha ya Pamoja Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana akiwa na Menejimenti Pamoja na wajumbe wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa.(picha na Mussa Khalid)
………………………
NA MUSSA KHALID
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana ameitaka Bodi ya Wakurugenzi Makumbusho ya Taifa kuonyesha jitihada za kuongeza idadi ya watalii ili kujipatia mapato ya kutosha mpaka 2025 yafike Dola za Kimarekani Bill 6.
Balozi Dkt Chana ameeleza hayo Leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Bodi ya Makumbusho ya Taifa ambapo amesema ni vyema pia Bodi hiyo ikahakikisha inasimamia Utamaduni wa Makumbusho ya Taifa ikiwa ni pamoja na kulinda ,kuhifadhi na kutangaza urithi wa asili na Utamaduni wa Nchi.
Aidha Balozi Dkt Chana ameitaka Bodi hiyo kwa kushirikiana na Menejimenti ya
Makumbusho kufanya kazi kwa juhudi na ufanisi mkubwa ili kuweza kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea.
“Sisi ni watu wa maadili na hivyo lazima tuweze kuyaendeleza kama kauli Mbiu yetu isemavyo tumerithishwa tuwarithishe lakini pia ukizingatia pia kuwa sisi wenyewe Watanzania ni kivutio cha utalii kutokana na maadili yetu na watu wanavyoishi hivyo wageni wanapokuja wanajifunza pia utamaduni wa Mtanzania anavyoishi “amesema Balozi Dkt Chana.
Balozi Dkt Pindi Chana amemshuruku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Kwa kuizindua Program ya Tanzania Royal Tour kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya watalii nchini.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Oswald Masebo amesema kuwa wao kama bodi wanatambua unyeti wa Taifa la Tanzania hivyo watahakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano Ili kuendeleza kuwavutia watalii wengi kwenda kufanya utalii Katika Makumbusho hizo.
“Msingi ya Bodi ya Makumbusho ni kusimamia utendaji wa Menejimenti ya Shirika ikiwa ni pamoja na kuhifadhi na kuendeleza urithi wa Utamaduni wa kihistoria katika Taifa la Tanzania na Utamaduni huu ndio urithi wa Taifa kwani ndio unaolitambulisha Taifa na kuleta taswira njema”amesema Masebo
Amesema Makumbusho ya Taifa ilianzishwa kimkakati kwa ajili ya kutunza na kuhifadhi misingi ya Taifa la Tanzania hivyo jazi ya Bodi ni kuchochea hamasa ndani ya Makumbusho hiyo Ili ichangie kuongeza fursa za kiuchumi Katika Taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa Bodi hiyo itasaidia kutoa mwelekeo wa kuisimamia Taasisi hiyo katika kuimarisha malengo yake kwenye maeneo ya hifadhi na Urithi wa Taifa lakini pia kuyaendeleza yaweze kufunguka ili kukuza sekta ya utalii.
Amesema Makumbusho ya Taifa awali ilikuwa ikipata watalii wachache chini ya Laki saba lakini kwa Mwaka huu baada ya uzinduzi wa Royal Tour wameweza kuwapata wageni wengi wa Kitaifa na Kimataifa na hivyo kujiongezea mapato zaidi.
Kaimu Mkurugezi wa Idara ya Malikale Dkt Emmanuel Bwasili amemuhakikishia Waziri kuwa Makumbusho zitaendela kupata manufaa kupitia Malikale zilizopo nchi kwa kuwashawishinna kuwavutia watalii kwenda kufanya utalii sambamba na kujifunza historia ya Tanzania