Sufiani Hussein Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) akiwaonesha waandishi wa habari sukari inayozalishwa katika kiwanda cha Bagamoyo Sugar kilichopo kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Sufiani Hussein Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) akiwaonesha waandishi wa habari mahali ambapo mitambo ya kuvuna maji yanayotumika katika kiwanda cha Bagamoyo Sugar imewekwa kando ya mto Wami.
…………………………………..
Mradi wa shamba la kulima miwa na kiwanda cha Sukari kinachojulikana kwa jina la Bagamoyo Sugar umekamilika Kwa asilimia kubwa huku uzalishaji wa sukari yenye chapa ya Azam ukiwa umeanza.
Hayo yamesemwa leo na Sufiani Hussein Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) mbele ya wanahabari walipotembelea katika kiwanda hicho cha Bagamoyo Sugar Limited kilichopo Zinga Bagamoyo huku akisema sukari hiyo imeanza kusambazwa na inapatikana kote nchini.
Bw. Sufiani ameishukuru serikali ya wilaya, mkoa na serikali Kuu kwa ujumla kwa kuwaunga mkono katika kufanikisha mradi huo, huku akisema mradi umegarimu dola za kimarekani milioni 110 ambapo kiwango chote hicho cha fedha kimepatikana kutoka kwenye taasisi za kifedha za kitanzania pamoja Kampuni mama ya Said Salim Bakhresa (SSB) akiongeza kuwa inaonyesha ni namna gani miradi mikubwa inaweza fadhiliwa na taasisi za ndani na ikafanikiwa kama Bagamoyo Sugar limited ilivyofanikiwa.
“Sukari yetu ya Bagamoyo Sugar imefungashwa kulingana na mahitaji ya wateja wetu kuna mifuko ya kilo hamsini (50) kuna mifuko ya kilo ishirini na tano (25) kuna kifungashio cha kilo moja pia kifungashio cha gram mia tatu na ishirini pamoja na gram mia moja hamsini tumefanya hivi ili kuwezesha wananchi kupata Sukari hii kwa uhitaji tofauti,” amesema Sufiani Hussein
Kwa namna nyingine ndugu Sufiani Hussein amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kutumia bidhaa za Kampuni ya Said Salim Bakhresa SSB huku akiwakaribisha kutumia bidhaa mpya ya Bagamoyo Sugar
Sufiani Hussein Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa SSB akionesha moja ya mtambo wa kuvuna maji kati ya mitambo mitatu iliyotegwa katika mto Wami kwa ajili ya maji yanayotumika kwenye kiwanda cha sukari cha Bagamoyo Sugar.
Mhandisi wa Umwagiliaji katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar Steven Peter Leo akionesha namna mitambo ya umwagiliaji katika kituo cha umwagiliaji mashamba inavyofanya kazi.
Mitambo ya umwagiliaji maji katika mashamba ya miwa katiia kiwanda cha Bagamoyo Sugar.
Mitambo ya uvunaji miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari kikiendelea na uvunaji.
Said Nassor Naibu Mkurugenzi Kiwanda cha Kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar akitoa maelezo katika eneo la kupokelea miwa kwa ajili ya uchakataji kabla ya kuzalisha sukari katika kiwanda hicho.
Muonekano wa baadhi ya mitambo.
Waandishi wa habari wakitembelea maoneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
Eneo linalozalisha umeme kwa ak za miwa ambapo Megawati 5 zinazalishwa kwa ajili ya kutumia kuendesha mitambo kiwandano hapo, kiwanda hicho kinatumia megawati 2 kwa uzalishaji.
Eneo ambalo mitambo ya kuzalisha sukari inakamilisha kazi ya kuzalisha na kutoa sukari.
Hapa baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika eneo la mwisho la kufunga sukari mara baada ya kuzalishwa kiwandani hapo.
Picha ya pamoja.