Mchezaji wa Filamu ya “Ndoto ya Samira”Samira Masoud akieleza dhamira ya kucheza filamu hiyo.
Afisa Elimu Mwandamizi Makumbusho ya Taifa Anamery Bageny akizungumzia namna filamu ya “Ndoto ya Samira”ambayo imeonyeshwa Katika Ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es salaam.Mume wa Samira Masudi bw.Mohamed Sheha Mohamed akieleza namna ambavyo wamekutana mpaka kushiriki katika filamu hiyo inayoeleza kisa Cha Ukweli.
Baadhi ya wanafunzi bao wamehudhuria katika onyesho Hilo la filamu ya Ndoto ya Samira ambayo imeonyeshwa Katika Ukumbi wa Makumbusho Leo jijini Dar es salaam.(Picha na Mussa Khalid)
………………….
NA MUSSA KHALID
Wanafunzi wanaopitia katika Mazingira magumu ya kuitafuta elimu wametakiwa kutokukata tamaa bali waongeze juhudi katika kujifunza ili kuzifikia ndoto zao.
Hayo yameelezwa leo katika uzinduzi wa filamu ya “Ndoto za Samira” ambayo imechezwa na Samira Masoud ikieleza Maisha halisi ya Samira tangu akiwa mwanafunzi shuleni ambao umefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam
Akizungumza katika Uzinduzi huo Afisa Elimu Mwandamizi Makumbusho ya Taifa Anamery Bageny mesema lengo la filamu hiyo ni kuwafundisha watoto wa kike waepuke kukata tamaa Ili waweze kufanikisha malengo yao waliyojiwekea kuanzia wanaanza elimu ya msingi mpaka vyuo.
Amesema Makumbusho ya Taifa itaendelea kuonyesha ushirikiano Kwa watanzania katika Mipango mbalimbali waliyojiwekea kwa kutoa elimu katika jukwaa linalopatikana kwenye Makumbusho hiyo hivyo ameitaka Jamii kutumia fursa hiyo kupenda kutembelea Makumbusho mara kwa mara ili waweze kujifunza historia ya nchi yao.
Awali akizungumzia Filamu ambayo ameicheza,Bi.Samira Masoud amesema Ndoto zake zilianza akiwa mdogo jambo ambalo likamsukuma kucheza filamu hiyo kwa lengo la kutoa ujumbe hasa Kwa wanafunzi wa kike kutokata tamaa Katika kuyatafita mafanikio.
Amesema wakati anafanya filamu hiyo amekumbana na changamoto Kwa baadhi ya watu wakidhani kwamba akipiga picha atakwenda kuwa muhuni kuuzwa.
“Tumeamua kuwalenga wanafunzi Kwa sababu ndoto ya mtu inaanzia akiwa mdogo hivyo nawashauri waendelee kujifunza Kwa bidii kwani hata Mimi licha ya kwamba niliolewa lakini niliziendeleza ndoto zangu na Sasa naisaidia familia yangu”amesema Samira
Aidha Msanii huyo ameishauri Jamii kutambua kuwa wanawake wanaweza kwani kumuelimiwha mwanamke Mmoja ni sawa na kuielimisha Jamii nzima.
Kwa Upande wao baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali wamesema filamu hiyo imewapa funzo la kutokata tamaa kwa wanafunzi huku wakiwashauri wanafunzi wenzao kusoma Kwa bidii Ili wafanikishe malengo yao.