Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo akizungumza na waandishi
wa habari wakati alipotembelea kujionea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST) yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo (mwenye tai) akiangalia
bidhaa mbalimbali za asili toka kwa wajasiriamali wa Tanzania wakati alipotembelea kujionea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST) yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo akizungumza na washiriki
wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki toka nchini Rwanda wakati
alipotembelea kujionea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki
(JAMAFEST) yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo akizungumza na washiriki
wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki toka nchini Tanzania waliokuwa na shindano la kukuna nazi wakati waziri huyo alipotembelea kujionea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST) yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo akifafanua jambo kwa
washiriki wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki toka nchini Uganda wakati waziri huyo alipotembelea kujionea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST) yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam
24 Septemba, 2019
*****************************
Na WHUSM –Dar es Salaam
24 Septemba, 2019
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo, amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam ili kujifunza Utamaduni wa nchi zinazoshiriki tamasha hilo.
Waziri Jaffo ameyasema hayo mapema hii leo alipotembelea maonesho ya Utamaduni wa Nchi za Afrika Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika
tamasha hili la Utamaduni ili kujifunza Utamaduni wa nchi mbalimbali zinazoshiriki
tamasha hili na hii ndio fursa pekee ya kukuza lugha ya Kiswahili ili kuunga mkono
juhudi za Mheshimiwa Rais,” Waziri Jaffo.
Aidha Waziri Jaffo amewakumbusha amesema kuwa tamasha hili ni la kihistoria hapa nchini kwani limekutanisha zenye Utamaduni tofautitofauti kwa wakati mmoja hivyo ni fursa kwa watanzania kujifunza mambo mbalimbali kama ususi, ushonaji, ngoma za asili na michezo mbalimbali.
Tamasha la JAMAFEST linashirikisha jumla ya nchi tano ambazo ni Kenya, Uganda,
Burundi, Rwanda na wenyeji Tanzania tamasha hilo linarajiwa kumalizika siku ya
tarehe 28 Septemba 2019