****************
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesaini mkataba wa miaka mitano (5) wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Tano Ishirini na Sita, Laki Moja Hamsini Elfu, Mia Moja Themanini na Tatu (Tsh. 526,150,183) na taasisi ya Save the Children Tanzania.
Kwa Mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na (THRDC) imesema mkataba huo umetiwa saini rasmi leo tarehe 12 October 2022 na utekelezaji wake utakamilika tarehe 30 October 2026 ukilenga kusaidia na kuimarisha shughuli za haki za binadamu nchini Tanzania
Fedha hizo zitatumika kuboresha shughuli za watetezi wa haki za binadamu hasa wanaotetea haki za watoto nchini Tanzania pamoja na kuimarisha kazi za watetezi wa haki za binadamu zikiwemo Asasi za Kiraia.
Save the Children ni moja ya Wadau wakubwa wa THRDC na Mdau wa Haki za Binadamu nchini Tanzania hasa haki za watoto.