NJOMBE.
Ikiwa Mwezi mmoja umesalia kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa kote nchini, Serikali wilayani Wanging’ombe imewakutanisha watendaji wa kata na maafisa tarafa na kutoa miongozo na taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika chaguzi hizo za kuwapata viongozi bora wa mitaa na vijiji.
Awali akizindua semina hiyo yenye lengo a kuwajengea uwezo watumishi hao wa umma mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge pamoja pamoja na Edward Manga ambaye ni katibu tawala wanawataka watendaji na maafisa tarafa kuzingatia Sheria zote za uchaguzi ili kupata viongozi wa wenye sifa huku pia wakitakiwa kutilega katika usimamizi wa amani katika maeneo yao.
Mara baada ya kupatiwa mafunzo baadhi watendaji na maafisa tarafa akiwemo Festo Mbakilwa na Adam Dononda wanaeleza jinsi watakavyoenda kuyafanyia kazi kwa maslahi mapana ya taifa huku wakitoa wito kwa wananchi kushiriki katika chaguzi hizo muhimu.
Wakati watumishi wakikiri kutekeleza kiapo chao katika, nae msimamizi wa uchaguzi wilayani Wanging’ombe Emmanuel Kilundo ambae ni afisa mipango anabainisha sifa za viongozi wanaopaswa kuchaguliwa .