******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kocha mkuu wa klabu ya Young Africa (Yanga) Mwinyi Zahera amesema wanajiandaa kikamilifu kwa mchezo ujao wa marudiano dhidi ya Zesco ya nchini Zambia utakaofanyika katika uwanja wa Revy Mwanawasa nchini Zambia ili kutinga hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika.
Zahera amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuwa mgumu huku akifahamu Zesco haijawahi kupoteza mechi nyumbani lakini watahakikisha wanavunja mwiko ili kutinga hatua hiyo.
“Kule Zambia tunahitaji bao moja tu ili kuingia hatua ya makundi, hatuna shida ya kufunga mabao 100 tukipata moja tu litatutosha na kutuvusha hatua hii,” alisema Zahera.
Katika mchezo wa hatua ya awali waliocheza na Township Rollers ya Botswana, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 nyumbani kabla ya kwenda kuifunga bao moja ugenini.