.
Na Silvia Mchuruza,Kagera;
Timu ya Kagera Sugar FC imewasili salama mjini Bukoba baada ya kucheza mechi tatu ugenini na kushinda mechi zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara huku ikiwa inaongoza msimamo huo.
Mara baada ya kuwasili imeingia kambini na kuendelea na mazoezi mepesi tayari kuziwinda pointi tatu muhimu dhidi ya wekundu wa msimbazi, timu ya Simba kutoka jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mecky Maxime,ametamba kuwa lazima Simba aacha tena pointi tatu kwani kikosi chake kipo tayari na mechi na wajipanga kuendeleza ubabe.
Ikumbukwe mwaka jana Kagera Sugar waliweza kuifunga Simba mechi zote mbili za Ligi Kuu Vodacom Tanzania hivyo anaimani kuwa ataibuka tena ushindi.
Hivyo Kocha huyo amewataka mashabiki wote wa Kagera Sugara na wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi na kuja kuona soka safi na wataondoka uwanjani kwa furaha na shangwe kama walivyofanya msimu uliopita.