Afisa Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bi. Bibiana Ndumbaro akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC walipotembelea katika banda la sgirika hilo kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
…………………………………..
Wananchi wa Mkoa wa Geita na Mikoa jirani wamezidi kumiminika katika banda la STAMICO katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Uwanja wa EPZA Bomba Mbili, Geita Mjini.
Wengi wa wananchi wanakuja kujionea jinsi Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes unavyo waka na hasa katika matumizi ya kupikia.
Mwaka huu STAMICO wamekuja kuonyesha kwa vitendo jinsi mkaa huu unavyowaka na unavyotumika kupikia (live cooking).
Mama Hamadi wa aliyetokea Chato amesema Mkaa huu ni mzuri jana nilinunua kilo moja kupikia Maharage hata haukumalizika na leo nimekuja kununua kilo mbili niende nazo Chato baada ya maonesho niweze kwenda kuutumia.
Baadhi ya watu waliohidhuria maonesho haya wamevutiwa jinsi banda la STAMICO lilivyopambwa pamoja na warembo wa Miss Coal Briquettes ambao wanalipamba banda hilo.
Leo ilikuwa Zanzibar Day (Blue Economy).
Maonesho haya yanatarajiwa kufungwa rasmi Jumamosi tarehe 08, Oktoba, 2022