********************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Oct 5
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Abdul Sharifu amewaasa wanachama wa CCM wilayani humo kuondoa matabaka na badala yake waungane kwa ajili ya Uchaguzi mkuu 2024-2025 ili Chama kiibuke na ushindi wa kishindo.
Ameeleza ,kwasasa wawe kitu kimoja hakuna mshindi bali mshindi ni CCM hivyo atakaebainika kuwagawa wanachama ,kamati ya maadili itawachukulia hatua kali.
Akipokelewa Kata ya Kisutu , na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Bagamoyo , alishukuru kwa ushindi alioupata na kudai hawatajutia .
Alisema, uchaguzi wa ndani ya Chama ngazi ya tawi -wilaya umekwisha ,na kilichobaki ni kujipanga kwa Kuwa wamoja kwa ajili ya ushindi 2025.
“Mama , Mwenyekiti wetu wa chama ana jambo lake 2025 ,ili tuweze kuendelea kushika dola, hakuna kubaki na visasi na nongwa wakati chaguzi zimeisha, kampeni ilikuwa ni vitu vya kawaida Kama tulikwazana tusameheane tugange yajayo”alifafanua Sharif.
Aidha alieleza , Mpango kazi wake ni kuhakikisha kila tawi na kata inakuwa na ofisi kwa ajili ya shughuli za chama kwani baadhi ya maeneo hazina ofisi.
“Kila kata itoe Mpango kazi wake wa ujenzi wa ofisi ,tuondokane na kukaa kwenye ofisi za chini ya miti au kupanga na kupewa ,tujitegemee Sasa, naomba mungu kwa kushirikiana na nyie wenzangu tukabadilike tuwe na ofisi zenye hadhi.”alibainisha Sharif.
Kwa upande wake mwakilishi wa madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo Salum Mikugo alisema kuwa watafanya kazi na mwenyekiti wao ili chama kisonge mbele.
Mikugo alisema kuwa wao kama madiwani watahakikisha wanaleta maendeleo kwa wananchi kwa kushirikiana na chama.