…………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana (Mb) amezulu Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kamabarage Nyerere lililopo Mwitongo wilayani Butiama na kuweka shada la maua ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kuenzi historian na mchango adhimu na adimu wa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amezuru kaburi hilo akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Mary Masanja (Mb), Uongozi wa Wilaya ya Butiama, Maafisa mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Taasisi nyingine.
Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana alikuwa wilayani Butiama mkoani Mara kuzindua na kushiriki mbio za hiyari zijulikanazo “Mwl Nyerere Marathon” zilizoratibiwa na Makumbusho ya Taifa nchini.