Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka BRELA, Bi. Rhoida Andusamile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini Madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma katika banda la BRELA kwenye maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.
……………………………
Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma kwa njia ya mtandao umewarahisishia wananchi kurasimisha biashara zao na kupata taarifa muhimu popote pale walipo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka BRELA, Bi. Rhoida Andusamile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini Madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma ya usajili kwa njia ya mtandao ( Online Registration System-ORS) kumekuwa na mwamko kwa watanzania kurasimisha biashara zao.
“Huduma za usaji kwa njia ya mtandao imewezesha kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma za BRELA popote walipo,” amefafanua Bi Andusamile.
Aidha ameongeza kuwa mbali na kutumia vyombo vya habari mbalimbali wameendelea kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha wananchi juu ya huduma mbalimbali za BRELA ili kuwa na uelewa wa pamoja.
“Hatuko nyuma kwenye suala la mitandao ya kijamii, tunaitumia ipasavyo kuhakikisha wananchi wanaelewa huduma tunazotoa,” ameongeza Bi. Andusamile.
Aidha amewasihi watanzania kurasimisha biashara zao kwa njia ya mtandao kwa kuingia kwenye wovuti ya BRELA.
“Mfanyabiashara anaposajili Jina la Biashara ama Kampuni, huaminika mahali popote na kupata fursa mbalimbali za kibiashara,” ameeleza.