………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Tanzania walioapishwa hivi karibuni na kuzungumzia namna Mabalozi hao watakavyo shirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika sekta ya Maliasili na Utalii Kimataifa.
Mabalozi hao ni Mhe. Balozi Saimon Siro (Zimbabwe), Mhe. Balozi Caroline Chipeta ( Uholanzi) na Mhe. Balozi Luteni Generali Mathew Mkingule (Zambia).
Kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi na Maafisa wengine wa Wizara ya Maliasili na Utalii.