Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo kuoka kwa Mhandisi Mshauri na Meneja Mradi Shabani Ndee wakati akimpatia maelezo Juu ya Ukarabati unahusisha kubadilisha madirisha,Milango,Makabati,Meza za Kusomea,Vyoo,Masinki ya Kufulia na Kunawia,Kusafisha Sakafu ,Kuweka Vigae Vyoo na Bafu ,Kubadilisha Mabomba ya Mfumo wa Maji Safi na Maji taka,Kuweka Upya Mfumo wa Umeme, Kuweka Upya Mfumo wa Maji ya Zimamoto na Kusafisha Kuta za Nje za Majengo yote Mawili.Hadi Sasa kiasi cha Tzs 1,722,929,930.34 kimeshalipwa kwa Mkandarasi SUMA JKT – NSCD.
(PICHA NA ADAM BENJAMIN -FULLSHANGWEBLOG)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwasili Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akikagua Mradi wa Ukarabati wa Mkubwa wa Mabweni Na. II na V unaotekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT – NSCD na Kusimamiwa na Kurugenzi ya Huduma Za Miliki ya CKD Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambao ulianza tarehe 26 Desemba 2018 na ulipaswa Kukamilika tarehe 24 Agosti 2019. Hata hivyo, Kutokana na Sababu mbalimbali,Mkandarasi hakuweza kukamilisha Kazi kwa Wakati na badala yake aliomba kuongezewa muda na kukubaliwa hadi tarehe 6 Oktoba 2019.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata Maelezo Juu ya Ujenzi wa Bweni II na kutembelea Sehemu Mbalimbali kwenye bweni hilo, na kuneshwa Mabomba ya maji yaliyokuwepo awali bwenini hapo takribani miaka 40 toka kujengwa, ukarabati huo pia umehusisha ubadilishaji wa mabomba na kuwekwa Mapya.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwasili Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi ya Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.
……………………………………………………………….
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema mabweni mawili ya wanafunzi maarufu “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu cha Dar es salaam yaliyokarabatiwa yatachukua wanafunzi 788 .
Profesa Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi ya Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.
Waziri huyo amesema mabweni hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 4.5, ambapo ukarabati huo umehusisha kuweka upya mifumo ya maji safi na taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya, madirisha uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.
Ukarabati huu wa mabweni hayo yaliyojengwa mwaka 1965 ulianza mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2019 na unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na kurugenzi ya milki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Waziri Ndalichako ameelezea kuwa ukarabati huo mkubwa wa mabweni hayo unafanyika kwa mara ya kwanza toka yalipojengwa baada ya kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.
Waziri Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia kazi za ukarabati katika chuo hicho.
“Nimefurahishwa na kazi hii ni bora na kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya 11,100. Naagiza uongozi mko hapa maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya kufunguliwa Chuo Novemba ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”
Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es salaam Profesa Wiliam Anangisye ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Waziri wa Elimu kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha imiundombinu ya chuo hicho ili kuhahakikisha vijana wanapata elimu katika mazingira bora.
Makamu Mkuu huyo amemuhakikishia Waziri Ndalichako kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika kwa wakati .
“ Tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia mapato ya ndani kuyaendeleza”
Nae Dr liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu shilingi bilioni 1.5 .
“ Napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi unahusisha majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi na bweni moja lililopo kitalu G. nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba mwaka huu“
Nae Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele, ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea Hall 5 na Hall 2 na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokaa chuo, kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwasili Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) College Of Electronic Technology ( CoET ) wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua ukarabati wa mabweni wa wanafunzi chuoni hapo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo katika moja ya bweni wakati alipokagua ukarabati wa mabweni Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akisaini kitabu cha wageni wakati alipofanya ziara Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akikagua Mradi wa Ukarabati wa Mkubwa wa Mabweni Na. II na V.