Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema Polisi waliokuwepo eneo la Inyala Mbeya waliwashauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga Fatma Omary na Dereva wake kutoondoa gari leo eneo hilo kusubiria Malori yapite ili magari madogo yaruhusiwe kama utaratibu unavyotaka lakini wawili hao walisema wana haraka hivyo wakaondoa gari hilo.
“Baada ya magari makubwa kuruhusiwa kupita magari madogo pia yaliruhusiwa ambapo Mkurugenzi alipofika mbele alihitaji kununua mahitaji hivyo akashuka na aliporudi kwenye gari akakuta muda wa kupita magari madogo umeshapita ikawa ni zamu ya magari makubwa, walipoingia katikati gari lilifeli breki likagonga gari la DED na mengine na kusababisha kifo cha DED, Dereva na Mtu mwingine mmoja”
“Wakati ameshuka Askari walimzuia wakamwambia ni muda wa malori lakini wakasema wanawahi, tunatoa wito mnapoambiwa msipite msubiri msipite mpaka Malori yamalizike, pale ni lazima tupite kwa kupishana kwasababu malori asilimia kubwa yanafeli breki ndio maana tunawasubirisha wanapita kwa awamu,